Jina : Consolata Lukosi
Umri : 20
Kutoka: Ilala
Kabila: Mhehe
Mwandishi : Tuelezee kidogo kuhusu Historia ya maisha yako?
Consolata: Mimi ni mtoto wa kwanza kati ya watoto watatu katika familia ya Bwana na Bi. Lukosi. Nilizaliwa mpanda mkoa wa Rukwa na baadaye kuhamia Mbeya na kujiunga shule ya msingi ya Isanga. Elimu ya sekondari nimeisoma Mbeya Secondary School, kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. Baada ya hapo nilihamia Dar es Salaam na kujiunga na Shule ya Sekondari ya Jitegemee, niliposoma kidato cha tano na cha sita.
Mwandishi: Ulianzaje fani ya urembo?:
Consolata :Ni fani ambayo nilikuwa naipenda sana tangu utotoni na pia ilikuwa ni kati ya malengo niliyodhamiria kufanikisha. Nilianza kufanya mambo ya urembo kupitia kitongoji cha Tabata niliposhiriki na kushinda Miss Tabata 2010. Baada ya hapo nilifanikiwa kuingia kambi ya Miss Ilala kuwania taji hilo, ambapo nilifanikiwa kushika nafasi ya tatu.
Mwandishi : Malengo yako ya baadae?:
Consolata : Ningependa kuwa mfanyabiashara wa kimataifa niliye na kampuni yangu binafsi na vilevile kuendelea kujihusisha na fani ya urembo hasa kupitia, uwanamitindo. Hivi punde nitajiunga na chuo cha Learn It ambapo nitachukua kozi ya biashara itakayoniwezesha kufanikisha lengo langu la kuwa na kampuni na kuwa mfanya biashara bora.
Mwandishi : Ni Kazi zipi unazofanya kampuni ya TBL kupitia kinywaji cha Redds ukiwa kama balozi wa REDD’s kwa sasa?
Consolata: Nianze kwa kusema nina furaha kubwa sana kuwa na bahati ya kuwa balozi wa Kinywaji cha Redds kwa mwaka wa 2010. Ninapokea kazi nzuri ya yenye heshima walizofanya wenzangu Victoria, Jokate na Natalia. Walikuwa ni mabalozi wazuri sana na kupitia ushauri na uongozi wao natarajia kufanya kazi itakayoleta mabadiliko kwangu na kwa jamii yangu na pia kwa Redds na kampuni ya Tbl.
Natazamia kufanya kazi kwa ukaribu sana na jamii hasa kupitia shughuli za kampuni mama ya kinywaji cha Redds, ambayo inatarajia kuanzisha miradi mablimbali ya maji nchini na vilevile kwa kuwa kinywaji cha Redds kinajihusisha moja kwa moja na kuimarisha sekta ya ubunifu na mitindo nitakuwa mstari wa mbele katika shughuli zitakazoihusiana na uimarishaji huu. Vilevile ninatarajia pia binafsi kuisaidia jamii yangu kwa kupigania haki za wanawake na watoto pamoja na kuielimisha jamii kuhusu kujiepusha na majanga kama Ukimwi na namna ya kujiepusha nayo.
Mwandishi : Nini unachoweza kuwaambia mamiss wengine au wasichana wengine walio kwenye fani ya urembo kwa ujumla?
Consolata : Ningependa wajue kuwa yahitaji sana moyo kuwa katika fani hii hivyo wasikate tama na kwa wale ambao hawakufanikiwa kufikia ngazi ya taifa wasisite kujaribu tena na pia waendelee kusoma na kujiendeleza katika shughuli za kuwaletea maendeleo wao na jamii inayowazunguka.
Mwandishi : Utajiepusha vipi na skendo mbali mbali zinazotolewa kwenye magazeti hasa zinazowalenga waliopo katika fani ya Umiss?
Consolata : Nitajitahidi kujiheshimu na kujilinda. Nitasikiliza ushauri wa Familia jamii na wakuu wangu kutoka Redds na zaidi kumuweka Mungu mbele.
Mwandishi :Unawaambia nini Watanzania au Jamiii kwa ujumla?
Consolata : Ningependa wategemee mambo makubwa na mazuri kutoka kwangu na pia natoa wito kwa wazazi wasiwakataze watoto wao kushiriki katika fani hii ya urembo bali kuwasupport.
Mwandishi: kwa sasa unaishi na nani?
Consolata :Ninakaa Yombo Vituka na Dada yangu mpendwa.
Kwa hisani ya full shangwe blogspot
0 comments:
Post a Comment