Social Icons

Friday, October 1, 2010

MAASKALI WAPYA WATUNUKIWA VYEO


Waziri Masha (mbele) akishuka jukwaani kwenda kukagua gwaride.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Lawrence Masha, jana amewatunuku vyeo vya Wakaguzi wa Polisi maofisa wa jeshi hilo waliohitimu mafunzo katika chuo cha maofisa wa polisi kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam. Katika mahafari hayo wahitimu walionesha kwa vitendo mambo mbalimbali waliyojifunza.


………Akikagua gwaride.


Kikosi cha bendera kikitoa heshima mbele ya mgeni rasmi.


Masha, akimvisha cheo cha Inspekta Msaidizi, WP Happiness Temu.


Aliyekuwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana (kushoto) akimweleza jambo mrithi wa nafasi yake, Suleiman Kova.


Wahitimu wakionesha ukakamavu.


………Wakionesha jinsi ya kumdhibiti adui mwenye bastola.


Kikosi cha kutuliza ghasia kikionesha jinsi ya kutawanya wafanya fujo kwa kutumia maji ya kuwasha.


IGP Mstaafu, Omari Mahita, akitaniana na Kamanda Tibaigana.


Kikosi cha kutuliza ghasia kikiwa tayari kwa kazi.

0 comments: