Social Icons

Friday, October 8, 2010

MISS PROGRESS ATINGA GLOBAL PUBLISHERS

MREMBO aliyenyakua taji la dunia kupitia shindano la kumsaka Miss Progress, Juliet William, mapema leo ametinga ndani ya ofisi za mtandao huu na kupata nafasi ya kujionea baadhi ya shughuli zinazofanywa na wafanyakazi wa kampuni hiyo.

MC George akiagana na Juliet.


Msanifu Kurasa wa magazeti mbalimbali ya Global Publishers, George Alphonce ‘MC George’ (kulia), akimuelekeza jambo Juliet, na aliye katikati ni Mhariri wa gazeti la Ijumaa Wikienda, Luqman Maloto.

Mwandishi wa kampuni ya Global Publishers, Hemed Kisanda(kushoto), akisalimiana na Juliet.


Mmoja wa wafanyakazi wa Global Publishers, Walusanga Ndaki (kulia), naye hakuwa nyuma kusaliamiana na mrembo huyo.
Msanifu kurasa wa gazeti la Ijumaa Wikienda, Huruma Bujiku (kushoto), akiongea jambo na Juliet muda mfupi baada ya kutembelea kwenye meza yake.

Muandaaji wa mtandao huu Clarence Mulisa (kulia) akiwa kwenye pozi na Juliet.
Richard Manyota (kulia) akimpatia Juliet, moja ya kadi yenye namba zake za simu.

Miss Progress, Juliet William (kulia) akiangalia baadhi ya habari zilizowahi kutolewa na magazeti ya kampuni hiyo na Mhariri Mtendaji wa magazeti hayo, Richard Manyota.


0 comments: