Rais Jakaya Kikwete akimlisha keki mmoja wa wajukuu zake usiku wa kuamkia leo kwenye hafla ya kuzaliwa kwake iliofanyika katika viwanja vya taasisi ya WAMA.,kulia kwake ni Mama Salma Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete akimlisha keki mkewe Mama Salma Kikwete usiku wa kuamkia leo,Mh Jk usiku wa kuamkia leo alikuwa anatimiza miaka 60.
Rais Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Clouds Media Group,Bw.Joseph Kussaga usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya taasisi ya WAMA,jijini Dar.
Rais Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd,Juhayna Ajmi.Rais Kikwete alipita kila meza kusalimiana na wageni waalikwa waliofikwa kwenye hafla yake fupi ya kusherehekea kuzaliwa kwake usiku wa kuamkia leo.
Rais Kikwete na Mkewe mama Salma Kikwete wakitakiana afya njema kwa kucheeers mbele ya wageni waalikwa usiku wa kuamkia leo,Rais Kikwete alikuwa akisherehekea siku ya kutimiza miaka 60.
JK akitoa shukurani kwa wageni waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo, na waandaaji wa shughuli nzima.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh Ally Hassan Mwinyi na Mh Pius Msekwa wakimpa mkono wa pongezi Mh Jakaya Kikwete kwa kutimiza miaka 60.
Mtoto wa Rais Kikwete,Ridhiwani, akimpa zawadi baba yake na kumpongeza kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa kwake,kwenye hafla fupi iliofanyika katika viwanja vya taasisi ya WAMA.
Mwenyekiti wa Prime Time Promotions,Juhayna Ajmi na Mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Clouds Media Grpup,Joseph Kusaga wakimpa mkono wa pongezi Rais Kikwete na Mkewe Salma Kikwete kwenye hafla hiyo.
Mtangazaji wa Clouds FM,Eprahim Kibonde akimkabidhi jezi ya timu ya Taifa ya Morroco Rais Kikwete ambayo wameitoa kama zawadi kwake.Timu hiyo itacheza na timu ya Taifa,Taifa Stars kesho katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Msanii mahiri wa kughani mashairi Mrisho Mpoto akitumbuiza kwenye hafla hiyo na kibao chake cha Adela, kilichowachangamsha wageni waalikwa waliofika usiku wa kuamkia leo kwenye hafla hiyo.
0 comments:
Post a Comment