Mkurugenzi wa Shear Illutions Shekha Nasser akizindua rasmi jarida la Shear kwa kutimiza mwaka mmoja,hafla hiyo ilikwenda sambamba na tukio la Shear Charity ball ndani ya hotel ya Double Tree,Masaki jijini Dar.
Mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia Juhudi za CCBRT katika kusaidia watoto wenye matatizo Bw. Januari Makamba, akizungumza mbele ya wageni waalikwa katika harambee hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree,Masaki jijini Dar. Januari Makamba amewataka watanzania kusaidia watoto wenye matatizo mbalimbali ili nao waweze kupata mahitaji mhimu kama watoto wengine na kuwapunguzia matatizo waliyonayo.
Mkurugenzi wa Shear Illutions Shekha Nasser, akisoma hotuba yake mbele ya wageni waalikwa mbalimbali katika harambee ya kuchangia juhudi za CCBRT kusaidia watoto wenye matatizo.
Mkurugenzi wa Shear Illusions,Shekha Nasser akibadilishana mawazo na mgeni rasmi January Makamba kwenye hafla hiyo.
Mratibu wa kampeni ya kutokomeza Malaria wa Zinduka,Mama Sadaka, akiwa katika meza ya pamoja na Msanii Mwasiti Alimasi ambaye pia ni mmoja wa mabalozi wa Malaria hapa chini,kushoto ni Zamaradi Mketema kutoka Clouds TV wakipata chakula cha usiku.
Mgeni rasmi katika tukio January Makamba akiwa na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima Absalom Kibanda ndani ya hotel ya Double Tree,Masaki jijini Dar.
Mkurugenzi wa Shear Illusions, akiwaongoza wageni waalikwa kupata chakula.
0 comments:
Post a Comment