LETICIA KAIJAGE (pichani kushoto, mwenye mkanda mweusi na blauzi ya njano) amefariki duania jana njioni jijini Dar es salaam. Leticia, alikuwa ni Afisa Habari wa kampuni ya matangazo ya ZK Advertising ya jijini Dar es salaam. Mtandao huu ulikuwa karibu sana na marehemu kutokana na kazi alizokuwa akizifanya za kuratibu shughuli mbalimbali za matangazo ya kampuni ya simu ya ZAIN. Uongozi na wafanyakazi wa Global Publishers unatoa pole kwa familia ya marehemu, wafanyakazi wa ZK na wa Zain Tanzania. Picha hii alipiga April 21 mwaka huu wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya Zain ya Uhuru wa Kuongea pale Makao Makuu ya Zain maeneo ya Morocco, Kinondoni na kufanyika shoo kubwa ya mwanamuziki kutoka Nigeria, J Martins. Mungu ndiye muweza wa kila jambo, ampokee mja wake na kumpumzisha kwa amani katika ufalme wake wa milele - Amina!
Picha hii marehemu alipigwa April 19, 2010 wakati wa Press Conference kuhusu ujio wa J Martins katika uzinduzi wa kampeni ya Zain - Uhuru wa Kuongea - Shilingi Moja!
0 comments:
Post a Comment