Meneja wa Huduma za Wateja kwa Zain Tanzania, Gabriel Kamkara, akifafanua jambo kwenye uzinduzi huo.
KAMPUNI ya mawasiliano ya simu za mkononi, Zain, leo imezindua promosheni itakayowazawadia wateja wake watakaosajili namba zao kabla ya zoezi hilo kufikia mwisho Oktoba 15 mwaka huu, dakika 30 za bure za muda wa maongezi.Akizungunza na wandishi wa habari mapema leo makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, Irene Mlola, alisema kuanzia leo mteja wa Zain atakayesajili laini yake atapatiwa muda wa hizo ambazo zitatumika ndani ya siku mbili ikiwa ni moja ya changamoto zinazotolewa na kampuni hiyo.
Ofisa Msimamizi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (TGB) Sadiki Elimsu (kushoto) akifutilia mchakato mzima wa tukio hilo. Katikati ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Zain, Gabriel Kamkara, na kulia ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, Irene Mlola.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mchakato mzima wa uzinduzi.
0 comments:
Post a Comment