RAPA ‘front line’ wa Bendi ya Extra Bongo ‘next level’, Grayson Semsekwa, anadaiwa kujiweka kwa ‘sistaduu’ mmoja wa kizungu ambaye jina lake halikuweza kuwekwa kwenye rekodi za Mateja20 mara moja.
Semsekwa alinaswa na kimwana huyo ndani ya Ukumbi wa Cine Club Mikocheni, Dar ambapo paparazi wa Mateja20 alifanikiwa kumkuta rapa huyo akiwa beneti na mzungu huyo na kubahatika kupenyeza kamera yake tayari kwa kumbukumbu ya picha.
Baada ya ‘polisi’ waMateja20 kuiweka ishu hiyo kiushahidi zaidi, alimfuata Semsekwa na kutaka kujua kulikoni, rapa huyo alishindwa kujibu moja kwa moja na kujikuta akionesha Utanzania wake kwa kumtwanga swali paparazi huyo kuwa kwani yeye anaonaje uwepo huo?
Hata hivyo, Mateja20 iliendelea kumkomalia kwa maswali lukuki ambapo Semsekwa alijikuta akiishiwa maneno na kukiri kuwa huyo ni mtu wake bila kutaja moja kwa moja kama ni mpenzi wake au laa.

0 comments:
Post a Comment