Social Icons

Wednesday, September 1, 2010

FM ACADEMIA YA CHOMOA MMOJA AKUDO!!!!!!

BENDI ya Muziki wa Dansi Bongo, FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, hatimaye imefanikiwa kumchomoa mpiga Gitaa kutoka kwa mahasimu wao, Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’, Pius Kamanyola, Mateja20 ina ‘full data’.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha safu hii, tukio la kumnasa mtaalam huyo wa Gitaa la ‘Ryhthm’ wa Vijana wa Masauti lilifanyika makao makuu ya ofisi za bendi hiyo wiki tatu zilizopita ikiwa ni mpango wa kujiandaa moja kwa moja na safari ya kuelekea uzinduzi wa albam yao mpya inayokwenda kwa Jina la ‘Vuta nikuvute, Mathematics Mayemba’.
Akisema na Mateja20 mwishoni mwa wiki iliyopita, ‘Prezdaa’ wa bendi hiyo, Nyoshi El- Saadat ‘Sauti ya Simba’ alisema kwamba kuanzia sasa anaomba mashabiki wao wote wakae mkao wa kula tayari kwa uzinduzi huo ambao utakuwa na mabadiliko makubwa kwa bendi hiyo.
“FM Academia ya sasa siyo kama uliyoiona miaka mitatu iliyopita, tumeamua kuzindua albam hii ya pili na utambulisho wa wanamuziki wetu wapya ili watu wategemee mabadiliko makubwa,” alisema Nyoshi.

0 comments: