Akiongea katika mahojiano mafupi na Mateja20 mmoja wa wahasisi wa kundi hilo Suma G, alisema kwamba awamu hii wamezamilia kufanya makubwa katika game la muziki wa Bongo, na kwamba tayali wameshaongeza safu ya washambuliaji na kundi kufikia idadi ya watu 8 tofauti na ilivyokuwa mwanzo.
Uboreshaji huo Suma G, alidokeza kwamba kutokana na mpango mzima wa kutobagua jinsia wamempa shavu mrembo mmoja ambaye watakuwa naye katika halakati za kusongesha kundi hilo hivyo suma G alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau wote wa muziki huo wakae makao wa kula tayari kwa mapambano kutoka kwao.
0 comments:
Post a Comment