Social Icons

Wednesday, September 15, 2010

DIAMOND MUSICA WAOMBOLEZA MSIBA WA P.DADY KIVYAO!!

Baadhi ya wanamuziki na viongozi wa Bendi ya Diamondi Musica, wakiingia kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar, ambako mwili wa aliyekuwa mkurugenzi msaidizi wa Diamond Musica, marehemu Perfect Kagisa 'P.Didy' ulizikwa. Tayali kwa maombi maalum kutoka kwa uongozi wa bendi hiyo mara baada ya kushuka Bongo jana wakitokea Arusha katika ziara ya burudani za sikukuu ya Idd.
Rapa machachari wa bendi hiyo Sauti ya Rad akibubujukwa machozi baada ya kuona kaburi la mkurugenzi wao.
Hapa wakipiga sala ya pamoja.
'Prez Daa' wa Bendi hiyo Mule Mule naye uzalendo ulimshinda na kujikuta akimwaga chozi.
Kaka wa marehem Kenny Kagisa (kushoto) akiwasha mshumaa katika makaburi hayo na wengine waliyoinama ni baadhi ya wanenguaji wa bendi hiyo wakiangua kilio makaburini hapo.
Hapa baadhi ya wanamuziki na mkurugenzi mkuu wa bendi hiyi Judis Moshi (kulia) wakisikiliza historia fupi ya marehem kutoka kwa Kenny, kwenye picha hii hayupo.
Wanenguaji wa bendi hiyo nawao hawakuwa nyuma kusikiliza historia fupi ya marehem, nyumbani kwao Kinondoni Manyanya jijini Dar es Salaam.

0 comments: