Social Icons

Wednesday, September 1, 2010

"ALI KIBA IS THE MAN OF MY LIFE" says Lulu!!

MCHEZA 'movie Star' Bongo mwenye umri mdogo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ au ‘Sidanganyiki’ (pichani) ameumwaga hadharani uhusiano wake na mwimbaji wa muziki wa Kizazi Kipya ‘Bongo Fleva’, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ huku akisisitiza kwamba ndiye atakayemwoa.
Lulu alianika siri hiyo alipokuwa akifanyiwa usaili na mtangazaji wa kipindi cha Take One, Zamaradi Mketema na kurushwa hewani na tivii ya Clouds Agusti 23, 2010.
Akibanwa mbavu na Mateja20 juzi Jumatatu kama kauli yake hiyo ilikuwa ya kutoka moyoni au alipenda kupeleka mbele ‘madakika’, Lulu alijibu haraka: “Nafikiri Ali Kiba ndiyo atakayekuja kuwa mume wangu, kwani nampenda na ni mtu wangu wa karibu kwa sasa.”
Baada ya msanii huyo mwenye mambo mengi kuliko umri wake kuamua kumwaga ugali, Mateja20 ililimsaka hewani Kiba ili naye asikike atakavyomwaga mboga.
Kwa upande wake, mbongo fleva huyo alikiri kumfahamu Lulu tena sana, lakini eti akadai kuwa, ni rafiki yake wa kawaida tu, hakuna uhusiano wowote wa kimapenzi.
Mateja20 haikuishia hapo, ilimminya vilivyo msanii huyo na kumuuliza anaichukuliaje kauli ya Lulu siku alipofanya mahojiano na kipingi cha Take Care cha Clouds Tv: “Ah! Naamini Lulu alikuwa anaufurahisha moyo wake, lakini hakuna ukweli wowote.”
Wakati huo huo ‘rekodsi’ za Lulu zinaonesha kuwa, miezi kadhaa nyuma, aliwahi kuripotiwa na moja ya magazeti ya Global Publishers kwamba, mrembo huyo na mlimwende Husna Maulidi aliyewahi kushiriki Miss Dar City Center 2009, walifikishana Polisi Magomeni, jijini Dar kwa kupigana, kisa kikiwa ‘kuibiana’ mwanaume aliyetajwa kwa jina la Kiba.
Hata hivyo, umri wa Lulu ambao unadaiwa ni miaka 17 umekuwa ukielezwa kuwa hastahili kufanya mambo anayoyafanya, wengi wakimtaka asome kwanza.

0 comments: