Social Icons

Saturday, September 18, 2010

DAR CITY COLLEGE YATOA MSAADA KWA MAYATIMA

Baadhi ya wanafunzi wa Dar City College, wakikabidhi misaada hiyo

Baadhi ya watoto wanaolelewa kituoni hapo wakiwa katika picha ya pamoja.

Mkurugenzi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Watoto Wetu, Ndugu Evans Tegete kilichopo Kimara Baruti jijini Dar es Salaam, akiongea na wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari cha Dar City College cha jijini
Dar Es Salaam.

Baadhi ya wanafunzi wa Dar City College wakimsikiliza Mkurugenzi huyo kwa umakini kabisa.


Mwanafunzi wa Dar City College, Rose Philbert (katikati) akibadilishana mawazo na mmoja wa watoto hao

Mtoto yatima, Neema Steven mwenye ulemavu wa ngozi, akiwa katika pozi na mwenzie aliyetambulika kwa jina la Happy Masuke.



WANAFUNZI wa chuo cha Uandishi wa Habari nchini, Dar City College, Jumamosi ya September 18 mwaka huu wamekabidhi msaada wa vyakula pamoja na sabuni za kufulia kwa kituo cha kulelea watoto yatima kinachojulikana kama Watoto Wetu, kilichopo Kimara Suka jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake mkuu wa msafara huo, Banisadry Omary ambaye pia ni katibu wa Society ya chuo hicho, alisema kwamba wao kama sehemu ya jamii wanaguswa na hali ya maisha ya watoto hao ambao wanalelewa katika kituo hicho, kwa kuanzia wameamua kutoa msaada wa Kilo 100 za unga wa sembe pamoja na mafuta ya kula lita 10 pamoja na boksi moja la mche wa Sabuni ya kufulia.


0 comments: