SIYO Stori kwamba star of Bongo Flavor Nassib Abdul ‘Diamond’ anatoka kimapenzi na ‘diva’ wa Kiwanda cha Muvi Bongo, Jacqueline Wolper, lakini picha ikisomeka hivyo mrembo mwingine ameibuka na kudai anaibiwa mali zake.
Mshiriki wa ‘shoo’ ya Maisha Plus Season 2, Upendo Moshi, ameanika kila kitu mbele ya Mateja20 kwamba alianza kujirusha na Diamond kabla ya kupata umaarufu alionao sasa, hivyo anashangaa Wolper kujimilikisha.
Akimwaga ‘mchuzi’ katika ‘one on one’ na Mateja20 Jumapili iliyopita, Upendo alisema kuwa alianza kusikia tetesi za kuwepo kwa uhusiano kati ya Diamond na Wolper kupitia watu wake wa karibu lakini alikuwa akiyapuuza maneno hayo.
“Maneno yaliendelea lakini baadaye magazeti yakaripoti. Nikaamua kumuuliza Diamond
lakini badala ya kunipa majibu ya maana aligeuka na kuwa mkali. Alifoka halafu akaondoka,” alisema Upendo na kuongeza:
“Nikiwa sina hili wala lile, baadaye tena akanitumia ujumbe wa simu kwamba mimi na yeye basi. Mimi najua haya ni matokeo ya Wolper.”
Hata hivyo, Upendo alisema kuwa ikiwa Diamond ataendelea na msimamo huo, hatokuwa na kinyongo, badala yake ataanza kuangalia ustaarabu mwingine.
Alipoulizwa na paparazi iwapo bado ana mapenzi na Diamond licha ya kukutwa na mkasa huo, Upendo alijibu: “Mimi najua bado nipo na Diamond, najua kinachomsumbua ni ujana, ila atarudi. Kwa upande mwingine moyoni nimeanza kuzoea.”
Mateja20 ilipomuendea hewani Diamond, alikiri kumfahamu Upendo lakini aligoma kuzungumzia chochote kuhusu madai ya yeye kusaliti penzi.
“Ndugu yangu mimi huyo mtu namjua lakini sipo tayari kuzungumza lolote kuhusu mambo yangu mimi na yeye, napenda kuzungumza mapya hayo yake yameshapita,” alisema Diamond.
Kwa upande wa Wolper, aliendelea kusisitiza kwamba hana uhusiano na Diamond, hivyo hajui lolote.

0 comments:
Post a Comment