Social Icons

Friday, August 27, 2010

LIL KIM ASAMBALATISHA NDOA YA MSHIKAJI DAR!!

WAKATI bado ‘memori’ ya shoo ‘hevi’ iliyoangushwa na staa wa muziki kutoka nchini Marekani, Kimbely Denise Jones ‘Lil Kmi’ katika Viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar wiki tatu zilizopita haijafutika, imedaiwa kuwa ujio wa nyota huyo umeipasua ndoa ya Hussein Nazir ’Pacha’ (25) na Shamsa Habib (22), wakazi wa Ilala.
Chanzo makini cha Ijumaa kilitonya kwamba, mapema baada ya Lil Kim kuondoka Bongo, gogoro kubwa liliibuka ndani ya familia hiyo baada ya mke, kunasa picha zinazomuonesha ‘my hazibendi’ wake akiwa amemkumbatia kimahaba mwanamuziki huyo wakiwa stejini.
Baada ya kuinyaka ishu hiyo kutoka kwa chanzo hicho makini, Mtandao bora wa Burudani Bongo, Mateja20 ulifunga safari hadi ofisini kwa mwanamke huyo ndani ya Mjengo wa Mliman City, Dar na kukutana naye ambapo bila kujali vituo wala koma, aliweka wazi dukuduku alilonalo kwa laazizi wake lililomfanya kuchukua uamuzi wa kufungasha virago na kurudi kwao.
Shamsa ambaye ndoa yake imetoa uzao wa watoto wawili, wa kike na kiume, alisema: “Ukweli ni kwamba nilipoziona picha za mume wangu akiwa amekumbatiana na Lil Kim, nilihisi uchungu moyoni kwakuwa nampenda sana.
“Nilimshaanga sana mume wangu kwenda kufanya jambo lile na kukata mauno mbele ya ‘kadamnasi’ huku tukiwa katika maandalizi ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.”
Katika hatua nyingine, Shamsa, mwenye asili ya Kiarabu aliongeza kwamba, siku zote amekuwa na nidhamu ya kutosha kwa mwenza wake huyo katika kuhakikisha ndoa yao inakuwa salama na yenye amani lakini kitendo hicho kilimkosesha raha na kuhisi kuna matukio mengi ya aina hiyo yanampita hivyo kunusa harufu ya usaliti kwa mumewe.
“Pamoja na kuniomba msamaha, bado jambo hilo linaniumiza moyo kwani hata siku moja sikutarajia mume wangu angefanya kitendo kama kile,” alisema Shamsa na kuongeza:
“Mbaya zaidi alinidanganya anakwenda kwenye biashara zake na hakutaka tuambatane, binafsi picha hizo nimeziona na kiukweli nimechukia sana.”
Hata hivyo, kwa mujibu wa wadau walioongea na Ijumaa, mwanamke huyo alitakiwa kuondoa shitaka moja la kukumbatiana na Lil Kim kwani ni jambo la kawaida kwa mashabiki kuserebuka na kupiga picha na msanii wa kimataifa kama huyo.
Wadau hao walimtaka Shamsa kushikilia shitaka moja la mumewe ‘kumchiti’ kuwa anakwenda kwenye biashara wakati alikuwa anakwenda kujirusha.
Kwa upande wake, Pacha, mbele ya Ijumaa nyumbani kwa familia yake Mtaa wa Sadani, Ilala Dar alikiri kutokea kwa ‘gogoro’ zito kati yake na mzazi mwenzake.
“Ni kweli ujio wa Lil Kim umeniachia machungu kwenye ndoa yangu,” alisema Pacha na kuongeza: “Nimejitahidi kuomba msamaha lakini nimeambulia patupu labda mnisaidie kuniuombea msamaha. Bado sijakata tamaa na nikifanikiwa nitawaambia.”


2 comments:

Anonymous said...

kazi kwelikweliiii
kazi ipoooooo!!!!!!!!!

Anonymous said...

jajajajaaaaa