Social Icons

Tuesday, May 4, 2010


Video ya nyimbo ya BATA kutoka kundi la Offside Trick imerudi tena kwenye TV baada ya kufanyiwa marekebisho yaliyohusisha kufutwa na kuzibwa kwa baadhi ya vipande 'Scenes' katika video hiyo vilivyosababisha video hiyo kupigwa marufuku kuonyeshwa kwenye vyombo mbalimbali vya TV. Hivi ni baadhi ya vipande vilivyofutwa katika video ya BATA version 2 'Clean version' ambayo imeishaanza kuonyesha kwenye baadhi ya vituo vya TV hapa Bongo.. Kupitia G5click.com unaweza kuona video zote mbili za Bata kwenye sehemu ya videos au unaweza kusachi kwa kuandika neno BATA MTAMU..

0 comments: