Social Icons

Friday, December 31, 2010

GLOBAL PUBLISHERS WAOMBA DUA YA KUFUNGA MWAKA


Baadhi ya wafanyakazi hao wakiwa kwenye maombi hayo.

WAFANYAKAZI wa kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Ijumaa, Risasi, Championi, Amani, Ijumaa Wikienda na Uwazi, asubuhi ya leo wamekusanyika pamoja makao makuu ya ofisi hizo eneo la Bamaga, Sinza, jijini Dar es Salaam, na kuendesha sala na dua ya kufunga mwaka wa 2010. Hili lilifanyika muda mfupi baada ya kumaliza kikao cha kupitia magazeti yaliyotoka leo.
Mtaalam wa IT wa kampuni hiyo Clarence Mulisa (kushoto), akishiriki sala hiyo na Mhariri wa gazeti la Amani, Hamida Hassan. Kushoto zaidi ni mkuu wa wachoraji katuni wa kampuni hiyo, Aloys James.
Mhariri wa gazeti la Championi Ijumaa, Elius Kambili (kushoto), akiwa kwenye pozi na Mhariri wa gazeti la Championi Jumatatu, Philip Nkini (katikati) muda mfupi baada ya maombi hayo kumalizika, na kulia ni mwandishi wa magazeti pendwa, Shakoor Jongo.
Mhariri kiongozi wa magazeti ya Championi, Saleh Ally (kushoto), akiwa kwenye pozi na wahariri wa magazeti hayo.

Mhariri mwandamizi wa magazeti ya GPL Paul Sifael (kushoto), akiwa kwenye pozi na Mhariri kiongozi wa Championi Saleh Ally (kulia) katikati ni msanifu kulasa wa magazeti hayo Latifa Sauko.
Latifa akiwa kwenye pozi na msanifu kurasa mwenzake Edna Titus ndani ya ofisi hiyo.
Mhariri wa gazeti la Championi Ijumaa Elius Kambili, akiwa kwenye pozi la pamoja na wasanifu kurasa wake.

LADY JAY DEE AZINDUA MAJI YENYE JINA LAKE


MWANAMUZIKI wa kizazi kipya Bongo, Judith Wambura (Lady Jay Dee) pichani, mapema leo amezindua maji yenye jina lake katika hafla ilifanyika Paradise City Hotel, jijini Dar es Salaam. Akiongea katika uzinduzi huo, Jay Dee alisema kwamba, anatarajia kuyaingiza maji hayo mtaani kuanzia Januari Mosi, 2011, na yatauzwa kwa bei ya kawaida. Alielezea pia namna atakavyoendesha shughuli zake za kibiashara na sanaa kwa ujumla. Akifafanua zaidi, alisema bendi yake itapunguza shoo ambapo sasa atapiga siku moja tu kwa wiki tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Maonyesho hayo yatakuwa yakifanyika kila siku ya Ijumaa katika ukumbi wa Mzalendo Pub Millennium Tower Kijitonyama, jijini Dar es Salaam. Pia Jay Dee, ambaye anakuwa mwanamuziki wa kwanza nchini kuwa na jina kwenye bidhaa kama maji, aligusia sula la kufanya kazi za kimataifa zaidi, likiwemo la kuingia mkataba na kampuni ya Rock Star, ambayo itasimamia kazi zake za muziki kwa muda wa miaka mitano.

Alimalizia kwa kusema kuwa mwanzoni mwa mwaka ujao, anatarajia kufungua mgahawa wake mkubwa maeneo ya Kinondoni-Morocco jijini Dar es Salaam, ikiwa ni moja ya mipango yake ya kimaendeleo kwa mwaka 2011.

Maji yaliyozinduliwa yakionyesha lebo yenye jina la Lady Jay Dee, muda mfupi kabla ya mchakato huo kuanza.

..maji na matamu!

Meneja wa Lady Jay Dee ambaye pia ni mumewe, Gardner Habash, akifafanua jambo katika uzinduzi huo.

Mwakilishi wa MTV na Rock Star Tanzania, Christine Mosha ‘Seven’ akifafanua jinsi mkataba wa JayDee na kampuni hiyo ulivyo.

Baadhi ya waandishi wa habari wa kike kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye pozi la pamoja.

Mpiga picha wa kampuni ya Habari Corporation, Muhidin Sufiani, akitimiza wajibu wake katika uzinduzi huo.

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Jaffary Mshamu ‘Jaffaray’ (katikati), akiwa kwenye pozi na baadhi ya wadau waliofika kushuhudia uzinduzi huo.

Mwanamitindo Fideline Iranga (kushoto), akiwa kwenye pozi na mwanamitindo wa kimataifa, Flaviana Matata, muda mfupi baada y

Lady Jay Dee wa (tatu kulia), akiwa kwenye pozi na baadhi ya waalikwa baada ya uzinduzi huo.

Afisa Uhusiano wa benki ya NMB, Shyrose Banji (kushoto), akiwa kwenye pozi na mtangazaji wa Star TV, Sauda Mwilima.

Baadhi ya wanahabari wakipata chakula cha mchana baada ya uzinduzi huo.


MATEJA20 WISH U HAPPY NEW YEAR



Wednesday, December 29, 2010

CHINA KUSAIDIA SEKTA YA SANAA NCHINI

Balozi muambata wa utamaduni wa China, Liu Dong akifafanua jambo wakati alipomtembelea Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego (Kulia) ofisini kwake Ilala,Sharif Shamba wiki hii.Katikati ni wakurugenzi idara mbalimbali za BASATA


Na Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeingia kweye makubaliano na ubalozi wa China nchini ya kubadilishana kazi za sanaa na wasanii mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha mashirikiano ya kiutamaduni na kukuza sekta hiyo nchini.
Akiwa katika ziara yake BASATA ambayo aliambatana na maofisa wawili wa ubalozi wake Huang Wei na Wang Hong,Balozi muambata wa utamaduni kutoka China,Liu Dong amesema kwamba nchi yake imejipanga kusaidia sekta ya utamaduni nchini kwa kuwashirikisha watanzania kwenye matamasha mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu ya sekta hiyo.
Bw.Liu alikubaliana kimsingi na BASATA katika kuimarisha mahusiano ya kiutamaduni ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kuwezesha ubadilishanaji wa kazi za sanaa na wasanii ili wapate fursa za kuuza kazi zao, kujitangaza na kushiriki katika matamasha mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.
“China kwa sasa inaweka nguvu kwenye suala la kubadilishana utamaduni baina ya mataifa haya mawili.Tunategemea kuwashirikisha wasanii wa Tanzania katika matamasha mbalimbali tutakayoyaandaa pamoja na kuwapeleka nchini China kwa ajili ya kuongeza na kubadilishana ujuzi” alisisitiza Liu huku akitaja sanaa za uchongaji, filamu, uchoraji, ngoma za asili, sarakasi na nyinginezo kuwa watazipa msisitizo.
Kwa kuanzia Balozi huyo wa China alisema kwamba,wasanii wa Tanzania watapata nafasi ya kushiriki matamasha na maonesho ya kuazimisha mwaka wa China ambayo yanatazamiwa kuanza mwishoni mwa Februari mwaka 2011 ambapo pamoja na wasanii kutoka Tanzania watakuwepo pia magwiji wa tasnia hiyo kutoka China pamoja na waandishi wa habari maarufu.
Kwa upande wake,Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alisema kwamba, ziara hiyo ya maofisa wa ubalozi wa China ambayo imekuja baada ya ile ya awali ya maofisa wa Baraza ubalozini kwao ni yenye manufaa makubwa na italeta tija kubwa katika tasnia ya sanaa na utamaduni kwa ujumla hasa ukizingatia wasanii wamekuwa na uhitaji mkubwa wa maonyesho na masoko ya kazi zao.
Alingeza kwamba,BASATA iko tayari kusaidiana na China katika masuala mbalimbali ya ukuzaji wa sekta ya sanaa huku akiweka wazi kwamba,uhusiano wa China na Tanzania ni wa muda mrefu sana hivyo kuna kila sababu ya kuuendeleza na kuuimarisha zaidi.
“Kama kuna suala lolote mtakalohitaji tuwasaidie katika kukuza ushirikiano wa kiutamaduni sisi tuko tayari na milango iko wazi.Bila shaka eneo hili la mashirikiano ya kiutamaduni ni nyeti sana na hatuna budi kulipa msukumo wa kipekee” alisisitiza Materego.

CHEKI VIJIMAMBO VYA BONGO BAANAAAA!!!

FM ACADEMIA KUPIGA MAKUMBUSHO MKESHA WA MWAKA MPYA

Prez Dar, wa Bendi ya FM Academia Nyoshi El- Saadat (katikati), akiongea jambo kwa waandishi wa habari, kulia ni meneja uhusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania Mutta mganyizi, mkurugenzi wa masoko wa Henken.

BENDI ya muziki wa dansi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma' inatarajiwa kufanya onyesho lake la mkesha wa mwaka mpya katiika ukumbi wa Kijiji Cha Makumbusho, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Mateja20 Meneja wa bendi hiyo Kelvin Mkinga alisema kuwa kama jinsi walivyofunika katika onyesho lao la X-Mas ndivyo itakavyokuwa siku ya mkesha huo ndani ya kijiji cha Makumbusho.
Mkinga aliongeza kuwa kiingilio cha onesho hilo kitakuwa sh. elfu kumi tu (10,000), kwa kila kichwa.
Baadhi ya wanenguaji wa bendi hiyo katika pozi.

KESI YA CHENGE YAMALIZIKA LEO!


Chenge akiwasili katika Mahakaman ya Kinondoni leo asubuhi kusikiliza hukumu yake.

Umati uliokuwa ukifutilia hatima ya Chenge uliokuwepo mahakamani hapo asubuhi.

Chenge akijitapa kiutani kuwa yeye ndiye “Rais wa Afrika” wakati akisubiri kusomewa hukumu. Kulia ni wakili wake, Simon Mponda.

Mke wa Chenge, Tina Chenge, (kulia) na ndugu zake, wakichekelea baada ya hukumu kutolewa.

Chenge akipongezana na mkewe baada ya hukumu.

Mke wa Chenge na ndugu wengine wakihesabu pesa kwa ajili kulipa faini.

Chenge na mkewe wakiondoka mahakamani hapo baada ya kesi kumalizika.

Awali, MBUNGE huyo wa Jimbo la Bariadi (CCM), alitiwa hatiani na Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa makosa manne, mawili yakiwa ya uzembe, mauaji na kuendesha gari lisilokuwa na bima na kuhukumiwa kulipa faini ya shilingi laki saba
baada ya kupatikana na hatia kwa makosa yote au kwenda jela mwaka mmoja
kwa kila kosa. Baada ya hakimu aliyekuwa akiendesha kesi hiyo, Kwey
Lusema, kutoa hukumu hiyo, upande wa mshitakiwa ulijikusanya na kulipa
faini hiyo na kuondoka na ndugu yao.

UZINDUZI WA ALBAMU YA TID WAFANA BILICANAS

TID akionyesha makeke yake katika uzinduzi huo.
MWANAMUZIKI wa kizazi kipya, Khaleed Mohamed (TID), usiku wa kuamkia leo alifanya uzinduzi wa albam yake inayokwenda kwa jina la ‘Sifai’ ikiwa ni ya nne katika mfululizo wa albam zake. Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Klabu ya Bilacanas na kuhudhuriwa na mashabiki wakiwamo mastaa kibao.

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Albert Mangwea ‘Ngwea’, akifanya makamuzi katika uzinduzi huo.

Mwanamuziki wa Hip Hop, Jaffary Mshamu ‘Jaffaray’ (kulia), akisalimiana na rafiki yake ambaye jina lake halikufahamika mara moja. Kushoto ni msanii wa filamu bongo, Chuchu Hans, akifutilia shoo hiyo.

Mshindi wa Big Brother 2009, Kevin Chuwang (kulia), akifuatilia uzinduzi huo na mchumba wake Elizabeth Gupta.

Kevin akionyesha uwezo wake wa kuchana mistari jukwaani katika uzinduzi huo.

Mmoja wa mashabiki waliofika ukumbini hapo akionyesha uwezo wake wa kukata nyonga.

Mwanamuziki Ambwene Yessaya ‘AY’ (kushoto), akikamua sambamba na TID.

LORI LA MAFUTA LA TEKETEA KWA MOTO MORO

Lori la mafuta likiteketea kwa moto eneo la Sangasanga, Morogoro.

LORI lililokuwa linasafirisha shehena ya mafuta ya petroli kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya, jana jioni liliteketea na moto kwenye msitu wa Mlima wa Mwarabu eneo la Sangasanga jirani na njia panda
ya kueleka Chuo Kikuu cha Mzumbe ambapo ni umbali wa kilomita 30 kutoka Morogoro
mjini.

Habari za awali zilizopatikana eneo la tukio zilidai kwamba lori hilo liliteketea baada ya kupatwa na hitilafu
ya umeme. Katika hatua nyingine, maafande wa kikosi cha Zima-Moto mkoa wa Morogoro, walizidiwa nguvu na moto huo baada ya magari yao mawili kuishiwa
maji huku moto huo ukiendela kuliteketeza gari hilo.

Tukio hilo ambalo lilivuta nadhari za watu wengi na kukwamisha kwa muda mrefu usafiri katika barabara hiyo, linaonekana katika picha ambazo zilinaswa na mtandao huu.

POLISI, CUF 'VITA' DAR ES SALAAM

Wafuasi wa Chama Cha Wananchi (CUF), wakiandamana kudai Katiba Mpya jana jijini Dar es Salaam.

ILIKUWA kama filamu kwa wakazi wa Dar es Salaam jana wakati baadhi ya viongozi na wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF), walipolizidi maarifa Jeshi la Polisi katika kuhakikisha wanafanikiwa kupeleka mapendekezo ya rasimu ya Katiba Mpya, huku risasi za moto zikitumika kujaribu kuwatawanya.
Awali juzi, Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, lilizuia kufanyika kwa maandamano hayo kwa madai ya kuwapo kwa mkanganyiko wa taarifa ya namna ya uwasilishaji wa rasimu hiyo iliyotumwa kwenda Jeshi la Polisi na Wizara ya Katiba na Sheria.
Kwa mujibu wa Kova, taarifa waliyoituma CUF kwenda Wizara hiyo, haikutaarifu kuwa wangepeleka mapendekezo hayo kwa njia ya maandamano huku iliyotumwa kwenda Polisi, ikisema kuwa wangepeleka kwa njia hiyo, jambo alilosema lilikuwa na tofauti ya maana.
Saa tatu asubuhi jana, wanachama wa CUF walianza kukusanyika katika Ofisi za Makao Makuu zilizopo Buguruni, Ilala, ili kuanza maandalizi ya maandamano hayo ambayo kimsingi yalikuwa kinyume cha sheria.
Wakiwa hapo, wanachama hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali na kutumbuizwa na muziki uliokuwa ukipigwa na magari mawili ya matangazo ya chama hicho huku wakizifuatisha, ukiwamo wa ‘kama noma na iwe noma sikubali leo narivenji mimi’ ulioimbwa na msanii wa kizazi kipya, Kaka Man.
Ilipofika saa nne, magari matano ya Polisi huku yakiwa na askari wa kutuliza ghasia, yalifika hapo na kuwataka wanachama hao kusitisha maandamo kama vile ilivyoagizwa; lakini agizo hilo lilipuuzwa na wanachama hao na kusisitiza kutimiza azma yao ya kuandamana hadi wizarani.
Ilipofika muda huo, maandamano hayo yalianza, lakini yakiwahusisha wanachama peke yao waliokuwa wakitembea kwa miguu na kubeba mabango mbalimbali huku viongozi wao, akiwamo Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Julius Mtatiro, wakikwepa kuungana na wanachama hao na kutumia magari mawili kuondoka eneo hilo na kwenda wizarani eneo la Barabara ya Sokoine karibu na Magogoni.
Aidha, maandamano hayo yaliyokuwa yakipita katika Barabara ya Uhuru, yalipofika Buguruni Malapa yalikutana na ulinzi mkali wa askari hao na ghafla umati huo ulitawanyika na kukimbilia mitaani baada kuliona gari maalumu la Polisi Namba PT 0886, lililokuwa limebeba maji ya kuwasha.
Baada ya kukimbilia huku na huko, baadhi ya wanachama hao walikutana na kuungana tena katika Mtaa wa Kilwa na kuendelea na maandamano hayo, hali iliyowafanya askari Polisi kufyatua risasi za moto zaidi ya saba hewani ili kuwatawanya.
Kutokana na hali hiyo, waandamanaji hao walikimbia kuelekea maeneo mbalimbali huku magari ya Polisi zaidi ya 10 yakikatiza katika mitaa hiyo ya Ilala kwa lengo la kuwatawanya wanachama hao ambapo pia ilifanikiwa kuwakamata wanachama wanne waliopelekwa katika Kituo cha Polisi cha Karume.
Akizungumza baada ya kukabidhi rasimu hiyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Oliver Mhaiki, Mtatiro alisema rasimu hiyo yenye sura 36, Ibara 130 na kurasa 88, aliyosema iliandaliwa kwa miaka minne, imezingatia mahitaji ya Watanzania wa sasa, hivyo ni wajibu wa Serikali kuipitia na kuifanyia kazi ipasavyo.
Alidai Watanzania wamechoshwa na Katiba yenye viraka inayowaongoza kwa sasa, hivyo rasimu iliyotolewa na CUF imezingatia mahitaji yote muhimu na kwamba ndiyo mkombozi kwa maisha ya Watanzania masikini.
Alidai chama hicho kinajiandaa kulidai Jeshi la Polisi Sh milioni 10 sambamba na kuandaa maandamano mengine kwa ajili ya jeshi hilo kwa kile alichodai kuwa limevuruga maandamano yao licha ya kulipatia taarifa tangu Desemba 21, mwaka huu kuwa litafanya maandamano hayo.
Akipokea rasimu hiyo, Katibu Mkuu Mhaiki alisema atayawasilisha mapendekezo hayo kwa Waziri wake, Celina Kombani, kama ambavyo chama hicho kilivyokusudia kufanya huku akiwaomba viongozi hao kuwa watulivu wakati taratibu zingine zikiendelea kufanywa na Serikali.
Kwa upande wake, Kova akizungumza jana juu ya tukio hilo, alisema Polisi hawana ugomvi na chama hicho wala hawakuwazuia kupeleka rasimu hiyo, isipokuwa walitaka wapeleke kwa njia ya kawaida na siyo maandamano kama walivyofanya jana.
Alisema Serikali ilishazungumza suala la Katiba Mpya kuwa linazungumzika na linafanyiwa kazi, kwa hiyo maandamano ya chama hicho cha upinzani hayakuwa na tija yoyote.
Alisema wametumia nguvu za wastani kuwatawanya wana CUF na watu tisa wanashikiliwa na jeshi hilo na hakuna aliyejeruhiwa katika maandamano hayo, na Polisi kupitia Idara yake ya Upelelezi inafuatilia suala hilo ili kuangalia hatua gani itachukua kutokana na kukiukwa kwa amri yao.

chanzo mwananchi