Social Icons

Thursday, June 30, 2011

MBUNGE WA VITI MAALUM ASITISHA MIKUTANO YA BUNGE

MBUNGE WA VITI MAALUM CHIKU ABWAO AVIPA KISOGO VIKAO VYA BUNGE AMUUGUZA MAMAYE MZAZI

MBUNGE wa viti maalum wa mkoa wa Iringa, Chiku Abwao, hatimaye ameamua kukacha shughuli za bunge na kwenda kumuuguza mama yake mzazi, Tatu Abdallahman (79), ambaye amerejeshwa hospitali na kutibiwa nyumbani kwake kijiji cha Gangilonga mjini Iringa.
Mgonjwa huyo anasumbuliwa na matatizo ya mshtuko wa moyo na umepelekea kupooza mguu wa kushoto na mkono.
Mbunge huyo Chiku Abwao ameshindwa kuhudhuria Vikao vya bajeti ya Serikali vianavyoendelea mjini Dodoma kwa siku kadhaa sasa kutokana na kumuuguza mama yake.

Wednesday, June 29, 2011

MPANGO MZIMA BONGO NIGHT

Msanii wa Bongo Fleva Steve William ‘R&B’ akirekodi wimbo studio, Kinondoni, Dar.

….Akiwa na msanii mwenzake, Edson Wilson ‘Baby Boy’.


Jamaa huyu (anayevuja damu mgongoni) ambaye ni dereva wa daladala amenusurika kifo baada ya kupigiwa mayowe ya mwizi na kupewa kipigo kidogo na wananchi sehemu za Bamaga-Mwenge, jijini Dar. Hata hivyo, ilibainika hakuwa mwizi.


Gari alilokuwa analiendesha dereva huyo.

Tuesday, June 28, 2011

DUKA LA KIMWANA WA TWANGA PEPETA 2011 LATAMBULISHWA

Asha Baraka akiongea jambo mbele ya waandishi wa habari.

Baadhi ya waandiishi wa habari wakishuhudia duka hilo.

DUKA la vipodozi linalotarajiwa kutolewa zawadi kwa Kimwana wa Twanga Pepeta 2011, limetambulishwa rasmi leo mbele ya waandishi wa habari, maeneo ya Kinondoni Studio, jijini Dar es Salaam, karibu na duka la Wasafi Classic.

Akiongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari, mkurugenzi wa mashindano hayo, Asha Baraka, alisema kwamba wameona ni vyema kuziweka wazi zawadi za washindi wa shindano hilo ili kuepusha utata wa aina yoyote.

Alisema zawadi zingine zitakazotolewa siku hiyo ni pamoja na Shilingi 500,000 kwa mshindi wa pili, Sh. 300,000 kwa mshindi wa tatu na washiriki wengine watapata kifuta jasho cha Shilingi 100,000 kila mmoja.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Julai 8 mwaka huu ndani ya ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.



Vimwana wakisikiliza wakati wa mkutano huo.

Msanii wa miondoko ya mchiriku, anayejulikana kama AT, akiongea mbele ya wanahabari.

Vimwana wakionyesha uwezo wa kunengua.

Asha Baraka akiwa ndani ya duka hilo.

Vimwana wakiwa kwenye pozi la pamoja.

LEMA AUKANA MUAFAKA WA UMEYA ARUSHA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Msingi wa Maendeleo ni Haki.

“Ninawasalimu wote .

Hivi karibuni, tarehe 21 Juni 2011 siku ya jumatano kuna taarifa nyingi
ziliandikwa katika vyombo vya habari kuhusu muafaka dhidi ya mgogoro
wa uchaguzi wa umeya uliokuwa unaendelea hapa mjini Arusha .

Ni kweli kabisa mgogoro wowote humalizwa kwa vikao na mashauriano, na
ndivyo ambavyo CHADEMA tumekuwa tukitaka toka awali na mimi binafsi
natamani tukae kwa amani katika nchi yenye misingi ya haki na utawala
wa kuzingatia sheria. Kimsingi kabisa tulitaka serikali ya CCM itamke
kuwa kosa limefanyika kwa kutozingatia kanuni ya uchaguzi wa umeya wa
Arusha na kupelekea hapa tulipofika.

Mchakato wa muafaka ulipoanza mwanzoni mwa mwezi APRILI 2011 ulikuwa
na nia ya kuitaka serikali ione makosa hayo na ichukue hatua kwa
wahusika waliosababisha kufika katika hali tata tuliyofikia sasa na
sio kufarijiana kwa vyeo. Mgawanyo wa nafasi au vyeo ni mapendekezo tu
yenye kutaka madiwani wote kushiriki utumishi kwa wananchi lakini
haikuwa msingi wa madai yetu.

Baada ya kufanya utafiti na kufikiria kwa makini juu ya mchakato wa
kufikia muafaka huu ndipo nilipogundua pamoja na nia nzuri ya CHADEMA,
serikali ya CCM haijachukulia kwa nia na dhati ya kweli ili kutoa
majibu ya msingi ya madai yetu kuhusu HAKI na KUZINGATIA KANUNI lakini
pia kuonyesha toba na ukiri wa makosa yaliyofanyika ili wananchi
waweze kutuelewa.

Kwa sababu ya muafaka huu kushindwa kutoa majibu ya msingi kwa kweli
siwezi kukaa kimya hata kidogo juu ya muafaka huu ambao ni
udhalilishaji wa utu wa Mwanadamu na haki kwa kiwango cha hali ya juu
sana na katika mambo ya msingi tuliyokuwa tunapinga katika suala la
umeya ni ukiukwaji wa haki , taratibu na sheria katika uchaguzi wa
umeya uilokuwa umefanyika Arusha Mjini pamoja na sababu nyingine hii
ilikuwa ni sababu ya msingi ya kupinga jambo hili hata tukaamua
kufanya maandamano tarehe 5/1/2011 yaliyopelekea watu watatu kuuwawa
kikatili na polisi na wengine zaidi ya 26 kuhumizwa vibaya huku
wakiachwa na vilema vya maisha.

Hatukupinga utaratibu huo ili tugawane vyeo na nafasi mbali mbali
katika manisipaa ya Arusha hili halikuwa lengo letu na kamwe haliwezi
kuwa lengo langu .

Hatukuwa tunampinga Meya wa Arusha kwa dini yake au kabila lake au
rangi yake tulipinga mfumo uliomchagua ambao ulikiuka utaratibu wa
msingi wa kanuni na sheria za uchaguzi pamoja na mambo mengi
yaliyohusu haki na usawa ,ukweli .

Tulisema Ocd wa Arusha aondolewe na polisi washitakiwe juu ya mauwaji
ya watu wasio na hatia na familia zao zilipwe fidia.

Tulitaka mkurugenzi wa manisipa ya Arusha aondolewe kazini kwa
kusimamia uchaguzi batili nakusababisha majonzi mengi na vifo vya raia
wasio na hatia.

Tulitaka uchaguzi wa umeya urudiwe hapa mjini Arusha na haki itendeke
na sio kugawana uongozi na mambo mengi ya msingi ambayo kila mtu
anajua na hata ulimwengu mzima unajua.
Hivyo basi siwezi kukubali dhambi hii na udhalimu huu eti tu kwa
sababu chadema imepewa unaibu meya kwani huu sio msingi mama wa
muafaka na kama suala ni unaibu Meya mbona tulimuona Diwani wa kata ya
Sokoni one Mh Kivuyo kuwa ni msaliti alipokuwa ni naibu Meya ?
Ninatambua na ninajua inaweza kuwa vigumu kueleweka katika hili au
kupewa tafsiri nyingi nyingi tu, napenda kujiweka wazi kuwa
nitasimamia ukweli daima kwa maslahi ya wananchi na niko tayari
kusimama na wananchi kukabiliana na upinzani wowote ili kuwatetea
maana mimi ni mtumishi wao kwani Haki na utu sio jambo la kupuuza na
kujadiliwa kwa vyeo au pesa.

Mwisho naomba mwenyezi Mungu anisaidie na watu wote wa Arusha mjini na
watambue mgogoro hauwezi kuzuia maendeleo ya Arusha Mjini hata kidogo
kwani hata bajeti ya 2011 -2012 ilipitishwa bila hata kuzingatia
kanuni na taratibu. Kuna wafanyabiashara wachahe wa Arusha
wanaoshawishiwa kuwa Haki hii tunayoitafuta inadumaza ukuaji wa
biashara zao, napenda kuwaambia kuwa Mgao wa Umeme, Ufisadi, Rushwa,
uonevu, kutokufutwa kwa kanuni na Ulaghai wa Serikali iliyopo
madarakani ndivyo vinavyodumaza uchumi wa Taifa na Chadema inapambana
ili kuhakikisha inajengwa Tanzania Mpya yenye kufuata Kanuni na
utaratibu na mfumo wa sheria utakaoleta Neema ya kweli Tanzania.

Ni nayo ilani yangu kwa wananchi wa Arusha nitatimiza kwa mipango yangu
na yale ya kisera yanayohusu Nchi nitaendelea kuongea kwa nguvu zote
kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutumia vyombo
vingine kama Mbunge.

Na pia niwaombe Madiwani Wafikirie kwa makini utashi wenu dhidi ya
jambo hili nimatumaini yangu mtakuwa mlifanya maamuzi kwa haraka sana
bila kiuzingatia ukweli.

Arusha nawaomba sana na mnapaswa kuwa wavumilivu na majasiri wakati
huu ambapo tunapita katika majaribu mengi katika kupigania
ukweli ,hatuwezi kuudhalisha utu wa mwanadamu na haki kwa kugawana
vyeo kwa kisingizio cha maendeleo, Hata hivyo hakuna maendeleo Duniani
yanayopita haki ,ukweli , utu , usawa ,na kama kuna mtu yeyote
anafikiri anaipenda Nchi yake basi awe mfano wa kufikiria na kutenda
Haki .

Msiogope Mungu yuko pamoja nasi Ukweli utashinda. Mungu Awabariki
sana.
GODBLESS J LEMA ( Mbunge Arusha Mjini )

KENYAN FATUMA NOOR NAMED CNN MULTICHOICE AFRICAN JOURNALIST 2011


Winner Fatuma Noor (left) and Collins Khumalo, President of MultiChoice Africa during CNN MultiChoice African Journalist 2011 Awards Ceremony.

Fatuma Noor from Kenya has been awarded the top prize at this year’s CNN MultiChoice African Journalist 2011 Awards Ceremony.

Fatuma Noor, who works for The Star Kenya, won for her investigative three-part series on the ‘Al-Shabaab’, which was chosen from among 1407 entries from 42 nations across the African continent.

The series tells the story of the young men who give up their freedom abroad to return and fight for the ‘Al-Shabaab’ in one of the world’s most dangerous places on earth – Somalia.

Fatuma Noor was one of the 27 finalists at the Awards ceremony on Saturday evening and was a winner in the category ‘General News Award (Print).’

The Awards, which rotate location each year in tribute to their pan-African credentials, were held at a Gala ceremony hosted by CNN and MultiChoice at The Sandton Sun Hotel, Johannesburg, South Africa yesterday evening, Saturday 25th June.

Nolo Letele, Executive Chairman MultiChoice South Africa and Parisa Khosravi, Senior Vice President of international newsgathering for CNN Worldwide presented Fatuma Noor with the Award.

Fatuma said: “I want to thank my mum and my boss Catherine, who believed in me when no one else did. There was a time in my life when I thought about giving up, but with this Award I'm not giving up any time soon”

Chair of the judging panel, journalist and media consultant Joel Kibazo said: “The judges were impressed with the high quality of entries to the competition this year, and this intrepid young journalist has shown great courage and determination in going the extra mile to tell this fascinating story. Fatuma Noor’s three-part series on the Al-Shabaab provides a detailed and personalised portrait of the young men who leave their comfortable western lives to join one of the world’s most ruthless militant groups in Somalia.”

Parisa Khosravi, Senior Vice President of International Newsgathering for CNN Worldwide, said: “Tonight’s journalists join an ever-growing community of excellence, each one representing the very best in African journalism. The collective talent celebrated here this evening is a sign of the increasingly assured voice in which Africa is telling its unique and myriad story. I congratulate them all."


Nolo Letele, Executive Chairman MultiChoice South Africa group said: “We are proud of our long-standing partnership with CNN for these awards. And we are even more proud to play a part in telling the stories of Africa. It is thanks to the excellence of these journalists that Africa has a voice on the international stage. Our warmest congratulations go out to the winners.”


Collins Khumalo, President MultiChoice Africa, said: “Congratulations to all the 2011 winners, we hope the acknowledgment you’ve received this year will inspire you to continue telling the African story to the world. Although there can only be one overall winner, we’d like to salute each and every journalist that entered. Without your hard work and support, the ongoing development of democracy and diversity of the media across the African continent would not be possible.”

The evening also recognised Mahamud Abdi Jama as this year’s recipient of the Free Press Africa Award, for his work in Somalia. His situation was noted by the Committee for the Protection of Journalists (CPJ) in New York. He wrote a critical article about the government there and was jailed for just over a month and released when pressure was put on the government of Somalia.

The CNN MultiChoice competition is now in its 16th year. The prestigious sponsors include: African Development Bank; Coca-Cola Africa; Ecobank, IPP Media, Tanzania; Ericsson; Merck Sharp & Dohme (MSD); Research In Motion (RIM), the company behind the BlackBerry® solution; South African Tourism and A24 Media. The Sandton Sun Hotel, Johannesburg is the delegate hotel for this year’s Awards.

The Awards’ 27 finalists from 13 countries enjoyed an all expenses paid five day programme of workshops, media forums, networking and had the opportunity to see some of the sights of Johannesburg prior to the Awards Ceremony.

Ways To Watch the African Journalist Awards:

Viewers across the continent and across the world will be able to watch the African Journalist Awards in the following ways:

  • M-Net will broadcast the ‘Highlights Programme’ of the Award Ceremony in July.
  • Broadcasters in 45 countries on the African continent will be transmitting the ‘Highlights Programme’ during July.
  • Internationally, the ‘Highlights Programme’ will be shown on OBE TV in the UK, The Africa Channel in the United States / UK and on RTP Africa.
  • CNN International’s longest-running feature programme, ‘Inside Africa’ will include a report on the Awards on Saturday 2 July at 1730 BST.

The overall CNN MultiChoice African Journalist 2011 wins a substantial cash prize, a visit to CNN Centre in Atlanta, to attend the three-week CNN Journalism Fellowship, along with the prize awarded to all category winners, which consists of a laptop computer, printer, a BlackBerry and a cash prize.

ATEMBEA JUU YA MAJI YA MTO THAMES JIJINI LONDON

Steven Frayne akitembea juu ya maji katika Mto Thames uliopo jijini London.

MBUNGE AILIPUA IKULU

Mbunge wa Chadema, Suzan Lyimo.
AHOJI SABABU ZA KUTENGEWA MABILIONI KILA MWAKA, MUUNGANO NAO WATIKISA BUNGENI
MBUNGE wa Chadema, Suzan Lyimo ameishangaa Serikali kwa kutenga mabilioni ya fedha kwa ajili ya ukarabati wa Ikulu ya Dar es Salaam kila mwaka, huku Serikali hiyo hiyo ikiendelea kusisitiza mikakati ya kuhamia Dodoma.

Akichangia mjadala wa bajeti kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na ofisi zilizopo chini yake, kwa mwaka wa Fedha 2011/12 jana, Lyimo alisema haungi mkono hoja hiyo, mpaka apewe majibu ya kuridhisha ya sababu za Rais kushindwa kuhamia Dodoma na badala yake kuendelea kutenga kiasi kikubwa cha fedha kukarabati Ikulu ya Dar es Salaam.

Akitoa takwimu mbalimbali za bajeti ya Ikulu tangu mwaka 2001 hadi mwaka 2011, Lyimo alisema kwa kipindi hicho cha miaka kumi, Ikulu imekwishatengewa zaidi ya Sh50 bilioni, fedha ambayo kwa maoni yake, zinatumika vibaya.

"Siungi mkono hoja hii kwa sababu tatu; moja ni ukubwa wa Baraza la Mawaziri, mbili uonevu wanaofanyiwa wanafunzi wa elimu ya juu na tatu Serikali kutokuwa na mpango wa dhati wa kuhamia Dodoma," alisema Lyimo alipoanza kuchangia mjadala huo.

Kwa mujibu wa mbunge huyo wa Viti Maalumu, kitendo cha Serikali kuendelea kuliomba Bunge liidhinishe matumizi ya Sh10 bilioni kwa ajili ya ukarabati wa Ikulu ya Dar es Salaam katika kipindi cha mwaka 2011/2012, kinaonyesha kuwa haina nia ya dhati wala utashi wa kisiasa kutekeleza mpango wa kuhamia Dodoma.

"Tangu mwaka 2001 hadi 2011, Ikulu hiyo imetengewa Jumla ya Sh56 bilioni. Kila mwaka Serikali inaomba Sh2 bilioni, mwaka jana iliomba Sh7.2 bilioni na mwaka huu imeomba Sh10 bilioni," alilalamika Lyimo na kuendelea:

"Hivi ni kweli mabilioni hayo yanatengeneza Ikulu ya Rais tu pale Dar es Salaam? Na kama kweli ni Ikulu, kwa nini isitengenezwe Ikulu ya Chamwino ili Rais ahamie Dodoma?" alihoji

Lyimo alisema haoni mantiki kwa Rais kuendelea kuishi Dar es Salaam wakati mpango wa kuhamia Dodoma ulianza tangu mwaka 1976 na kila mara Serikali imekuwa ikiendelea kusisitiza mpango huo.

"Mheshimiwa mmoja hapa alipendekeza Spika ahamie Dodoma, mimi nasema sio Spika ni Rais ndiye anayepaswa kuja Dodoma. Na kama Rais anahamia Dodoma hakuna waziri atakayebaki Dar es Salaam. Tunamtaka pia Waziri Mkuu kuja Dodoma," alisema.

Baraza ni mzigo
Kuhusu Baraza la Mawaziri, Lyimo alisema ni kubwa kupita kiasi na kwamba Serikali inapaswa kulipunguza ili kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima serikalini.

Alisema mawaziri 54 waliopo sasa, ni wengi mno na wanaiongezea mzigo wananchi ambao ndio wanaobeba jukumu la kuigharimia Serikali yao.

"Baraza la Mawaziri ni kubwa mno, wako 54 ukimjulisha na Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Rais wa Zanzibar. Nchi tajiri kama Marekani ina mawaziri 15 tu, kwa nini Tanzania ambayo ni maskini iwe na mawaziri wote hao?" alihoji na kusisitiza, "tunaomba Serikali iliangalie upya baraza lake la mawaziri."

Katika hoja ya uonevu aliodai unafanywa na Serikali kwa wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu, Lyimo alihoji sababu za wanafunzi kufukuzwa baada ya kufanya migomo na maandamano wakati kisheria, inaruhusiwa vyuoni.

Muungano watikisa
Katika hatua nyingine, hoja ya Muungano jana ilitawala mjadala huo unaoendelea bungeni baada ya wabunge kadhaa kutoka Zanzibar, kueleza kuwa bado una kero nyingi na hivyo kupendekeza uvunjwe.

Wakichangia mjadala huo kwa nyakati tofauti, wabunge hao walisema Muungano bado ni kero kwa Wazanzibari kwa kuwa kuna mambo mengi ya msingi ambayo yanatendeka bila kujali maslahi ya pande zote mbili.

Mbunge wa Mgogoni, Kombo Khamis Kombo alihoji namna haki inavyoweza kutendeka katika mazingira ya nchi hizi mbili kuungana kwenye wizara sita tu kati ya wizara 26 zinazounda Serikali ya Muungano.

"Seriklai hii ina wizara 26 na wizara za Muungano ni sita tu. Mambo yote yanayofanywa kwenye wizara ambazo sio za Muungano bajeti yake inapangwa na kutekelezwa na Serikali ya Muungano, sasa licha ya jambo hilo kuwa kikatiba, kutakuwa na usawa gani kati ya Zanzibar na Tanganyika?" alihoji.

Mbunge huyo alisema haamini kama Serikali ya Muungano ina nia ya dhati katika kutatua kero za muungano na kama ina nia ya kweli, iwajengee imani Wazanzibari kwa Waziri Mkuu kuzungumzia kero hizo wakati anajibu hoja za wabunge katika mjadala unaoendelea.

"Mheshimiwa Spika, katika mazingira haya, tunawahakikishia Wazanzibari kuamini kuwa Tanganyika (Tanzania Bara) inawadhalilisha. Zanzibar kuna mabalozi wanne tu tena wanapelekwa kwenye nchi za Kiarabu na sasa China amepaelekwa mheshimiwa Mapuri. Wazanzibari wana haki, uwezo na haki ya kupeleka wafanyakazi katika balozi,"alieleza.

Kombo alisema kitendo cha Serikali kupuuza mapendekezo ya kamati ya Nyalali, Shelukindo na Amina Salum Ally kuhusu kero za Muungano ni ishara tosha kwamba haina nia ya dhati kutatua kero hizo zinazolalamikiwa na Wazanzibari.

Maelezo hayo yaliungwa mkono na mbunge wa Micheweni (CUF), Haji Khamis Khai aliyeeleza kuwa Wazanzibari hawana imani na Muungano huo kwa kuwa wao ni maskini kuliko Tanzania Bara.

"Kama Zanzibari ni mzigo kwenu (Bara) tuvunje muungano huo, mtuache," alisema.

Alisema inaudhi Wazanzibari kuzungumzia kero za Muungao kila siku na Serikali ya Muungnao ikiendelea kuwa kimya bila kutoa kauli inayotekelezeka."Tunaomba Muungano uvunjwe na uundwe tena kama ni lazima," alisema.

Hii ni mara ya pili kwa wabunge kujadili hoja ya Muungano katika Mkutano huu wa nne unaondelea sasa. Mara ya kwanza hoja hiyo iliibuliwia na mbunge wa Chwaka (CCM), Yahya Kassim Issa ambaye aliliambia Bunge kwamba Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar, bado una sintofahamu nyingi.

Akichangia Hotuba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda Kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Bunge ya mwaka 2011/2012 jana, mbunge huyo alisema suala la Muungano bado lina utata unaopashwa kushughulikiwa haraka.

"Mheshimiwa Spika, Wakati Rais akitolea ufafanuzi suala hilo la Muungano alieleza kuwa Zanzibar ni nchi ndani ya nchi ya Tanzania lakini, Nje ya nchi, nchi ni Tanzania. Lakini mheshimiwa spika, mpaka leo vitabu hivi, bado vinaitambua Zanzibar kuwa ni mkoa kama ulivyo Kilimanjaro!"

"Mbona vitabu havitoki kubadilisha hilo ili Zanzibar isomeke kuwa ni nchi kama Rais alivyosema? Huu ni mzozo, Zanzibar kuonekana kama mkoa na sisi (Wazanzibari), hatutaki," alilalamika.

JUISI YA KITUNGUU: HUPONYA YALIYOSHINDIKANA HOSPITALI!

Katika makala ya leo nawaeleza faida za juisi ya kitunguu maji katika mwili wako, ikiwemo uwezo wake wa kuzuia na kutibu magonjwa sugu na yaliyoshindikana kwa kutumia dawa za hospitali.

Tunapaswa kutambua kwamba viungo vingi tunavyotumia jikoni kwenye vyakula vyetu kila siku vina uwezo mkubwa wa kuponya magonjwa yanayotusumbua. Sina shaka kama kuna mtu ambaye hakijui kitunguu, nyanya, au kitunguu saumu.

Kitunguu maji ni kiungo cha mboga, ambacho aghalabu hutumika katika mapishi ili kuongeza ladha katika chakula na wakati mwingine hutumika kutengenezea kachumbari. Baadhi ya watu hawapendi kula kachumbari kwa kutokujua umuhimu wake mwilini.

KITUNGUU KINATIBU YAFUATAYO
Katika orodha ndefu ya magonjwa yanayotibika PASIPO SHAKA kwa kutumia juisi ya kitunguu, ni pamoja na ugonjwa unaowasumbua watu wengi wa kutokwa na damu sehemu ya haja kubwa wakati wa kujisadidia.

Ugonjwa huu, ambao kwa kitaalamu unajulikana kama ‘hemorrhoids’ au ‘Piles’, unawatokea watu wengi ambao kama mtu hukupata nafuu kwa kula vidonge, suluhisho la mwisho huwa ni kufanyiwa upasuaji mdogo katika njia ya haja kubwa, upasuaji ambao huambatana na maumivu makali.

Kwa wale ambao wameshakutwa na tatizo hili au wanalo hadi sasa, dawa kama vile ANUL SUPPOSITORIES, SECNIDAZOLE, n.k zinajulikana sana kwao, kwa sababu ndiyo dawa zinazopendekezwa na madaktari wengi kutumiwa ili kutibu PILES. Unaweza ukapona kwa muda na tatizo likajirudia baadaye au unaweza usipone na ukalazimika kufanyiwa upasuaji.

Lakini kwa kutumia juisi ya kitunguu, unaweza ukapona kabisa na inawezekana tatizo lisijirudie, kwani mzizi wa tatizo huondoka kabisa kutoka tumboni.

SIFA YA KITUNGUU
Kitunguu kina virutubisho vyenye uwezo wa kuua bakteria (antibacterial) na fangasi mwilini. (anti fungus). Pia kina virutubisho vyenye uwezo wa kuzuia wadudu wanaosababisha magonjwa nyemelezi (anti free radicals) na magonjwa ya uvimbe (anti informatory).

Mbali na sifa hizo, kitunguu kina kiwango kikubwa cha madini kama vile ‘calcium’, ‘magnesium’, ‘sodium’, ‘potassium’, ‘selenium’, ‘phosphorus’ na bila kusahauu kiasi kidogo cha aina fulani ya mafuta ambayo huimarisha kinga ya mwili.
JINSI YA KUJITIBU ‘HEMORRHOIDS.’

Kama nilivyoanza kusema awali, pamoja na magonjwa mengine yanayotibika kwa kitunguu, leo tutaanza kwanza na ugonjwa huu unaosumbua watu wengi. Dawa hii ni ya uhakika kwa mtu atakayeweza kuitumia kama inavyotakiwa.

Kunywa juisi ya kitunguu kila siku asubuhi kwa muda wa siku saba hadi siku 14, ikitegemea na ukubwa wa tatizo lako. Juisi hiyo lazima uinywe asubuhi kabla ya kula kitu chochote (on empty stomach) na utaruhusiwa kunywa kifungua kinywa chako saa moja baada ya kunywa juisi hiyo.

Dozi hii ni maalum kwa ajili ya kutibu ‘hemorrhoids’, ingawa wakati ukitibu tatizo hilo, matatizo mengine yaliyomo mwilini yatakuwa yakijiondoa, kama tutakavyoona katika makala haya wiki ijayo. Napenda kukuhakikishia kuwa tiba hii ni ya uhakika na haina madhara yoyote.

TAHADHARI
Mara baada ya kuinywa juisi hii kwa mara ya kwanza na siku chache zitakazofuata, utajisikia vibaya na tumbo kuchafuka. Hali hii ni ya kawaida, unachotakiwa kufanya mara baada ya kunywa, ni kukaa au kulala kwa muda, baada ya muda hali yako itarejea kama kawaida. Baada ya siku tatu, ukinywa mwili utaizoea na utajisikia kawaida tu.
Itaendelea wiki ijayo.

HII NI KWELI?

JE, umewahi kuona bilula “inayotema” maji bila kuliona bomba lake linakotokea?
Kwa ufahamisho tu ni kwamba, “bilula” ni kile kidude kilicho mwisho wa bomba linalobeba maji ambacho hutumiwa kulifunga au kulifungua ili liweze kutoa maji.

Neno hilo ni Kiswahili murua japokuwa cha zamani.
Turejee kwenye swali letu: Umewahi kuliona bomba (bilula) linalotoa maji bila kujua au kuyaona maji hayo yanatokea wapi?

Kama hujawahi kuliona, basi ni hilo linaloonekana katika picha hii. Bilula hiyo iko sehemu inayoitwa Aqualand, Hispania, ni moja ya vivutio vikubwa duniani ambapo watu hufurika kwenda kushangaa. Ni kivutio cha utalii.

Dude hilo ni kubwa na refu kwenda juu ambalo “hutema” maji kwa wingi kama vile yafanyavyo mabomba lukuki, kwa mfano, jijini Dar es Salaam, ambayo hunyonya maji kutoka Mto Ruvu ulioko mkoani Pwani.

Kweli, ni uchawi wa mchana kweupe!
Hata hivyo, ukweli ni kwamba: Hapa hapana uchawi wowote. Katika sehemu inayotoa maji kuna bomba lililofichwa na maji hayo ambalo hunyonya maji hayo kutoka chini, likayarushwa juu halafu yakateremka tena kama vile “yanatemwa” na bilula hiyo!

Inafurahisha, au siyo? Si uchawi, hata wewe unaweza kufanya hivyo! Ni uchawi wa kisomi.

MAMBO YA TWANGA LEADARS CLUB

Rapa wa bendi hiyo Diouf (kulia), akiwa na wadau wa bendi yake.

KAMERA ya mtandao huu ilijitupa katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam, ambako ilikusanya uhondo ufuatao katika picha ambao ulikolezwa na bendi ya Twanga Pepeta ya jijini:



Kipa wa zamani wa timu ya Yanga ya Dar, Nelson Kimathi, akiwa chobingo na mpenzi wake.


Wadau wa burudani wakifurahia shoo ya Twanga Pepeta.


Wasanii wa maigizo, wakijiandaa kuondoka uwanjani baada ya shoo kumalizika.

MAMBO YA TUZO ZA ZIFF ZENJI


Waigizaji waliofika katika tamasha wakiwa katika picha ya pamoja.
TUZO za msanii bora wa filamu nchini zimetolewa katika tamasha la kimataifa la filamu (ZIFF) lililomalizika jana huko Zanzibar ambapo kwa Muigizaji Bora wa Mwaka, tuzo hiyo ilienda kwa Jacob Steven ‘JB’ ambaye alijinyakuliwa tuzo ya dhahabu kupitia filamu yake ya Senior Bachelor, ambapo Filamu Bora ya Mwaka ilikuwa ni Ray of Hope iliyotengenezwa na Pilipili Entertainment chini ya mwandaaji Sajni Srivastava.


Msanii wa filamu, Jacqueline Wolper akifuatilia utoaji tuzo.

Mwanamuziki Cissoko kutoka Senegal akitumbuiza katika hafla hiyo.

Sajni Srivastava akionyesha tuzo aliyoshinda.

Jennifer Kyaka ‘Odama’ na Jack wakishuhudia tuzo hizo.

Mwanamuziki ambaye pia ni muigizaji, Baby Madaha, akiongea jambo katika hafla hiyo.

Mwigizaji Hashim Kambi akishuhudia mchakato mzima.

Timu ya Pilipili Entertainment ikiwa katika picha ya pamoja.

Hashimu kambi na Natasha.

Sajni na Baby Madaha.

Kanumba na Steve Nyerere.

Anti Ezekiel naye alikuwepo.

Baby Madaha akiwa na vijana wa Kizenji.


Friday, June 24, 2011

THE MAKING VIDEO OF " KAMA CHANGU YA MO` ROCKA

Usiku huu hapa Irish Pub kwenye video mpya ya Mo Racka akiwa amemshirikisha Jux, wimbo unaitwa KAMA CHANGU NITAPATA ambao umetengenezwa katika studio ya B'Hits chini ya Producer Pancho.


Jux akiwa katika poz

Dir Eryn akiwa na Izzo B wakikagua mzigo ulivyokuwa ukienda


Huyu shhhh... na huyu salute....iko pouwa hiyo