Social Icons

Sunday, July 31, 2011

KIVAZI CHA LINAH CHAWA KIVUTIO FIESTA 2011

MSANII wa miondoko ya Hip Hop kutoka nchini Marekani Ludacris, Usiku wa kuamkia leo alifanya makamuzi ya kutosha ndani ya Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam, ambapo aliingia nchini tangu Julai 28 mwaka huu, kwaajili ya kutumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2011, ambalo hufanyika kila mwaka.
Enesho hilo lililokuwa limesheeni wasanii kibao wa hapa nchini, lilikonga vilivyo mioyo ya mashabiki wake.

Kivutio pekee kilichosisimua tamasha hilo, nipale alipopanda msanii wa kike kutoka THT, Estalina Sanga 'Linah' akiwa ametinga kivazi kilichokuwa kikionyesha wazi baadhi ya maumbile yake.
Sambamba na hayo yote pia shoo hiyo ilivutia sana baada ya watangazaji wa Cluods FM, Fatma Ramadhani 'DJ Fetty', Adam Mchomvu na Hamisi Mandi 'B12' kushindana kwa kupiga na kuimba nyimbo za wasanii waasisi wa Bongoflava nchini, ambapo tamasha hilo lilikuwa likitimiza mika 10, tangu lianzishwe.
Ludacris akikamua jukwaani na jamaa yake.



Linah na kivazi kilichowavutia mashabiki zake
Gardener Habash akipokea tuzo kwa niaba ya Lady Jaydee kutoka kwa Linah.
Linah akiondoka jukawaani hapo.
Meneja wa kundi la TMK Family Saidi Felly (wa pili kulia),akiwa kwenye pozi na wasanii.

... mpango mzima ulihudhuliwa na umati wa kutisha.
Linah akionyesha uwezo wake.
Linah alipagawisha namna hii.
Mtangazaji wa kipindi cha XXL cha Clouds FM, Adam Mchovu akipagawisha mashabiki.
B12, naye alipagawisha kama Ludachris, mavazi hadi swagger zake.
Linex akikonga nyoyo za mashabiki waliojitokeza kwenye tamasha hilo.
Bob Junior, akitetea jina lake.
Shetta naye hakuwa nyuma kuwapagawisha wapenzi wake.
Mr Blue a.k.a Babaisa akikumbushia enzi zake jukwaani.
Dully Sykes, kulia, na wacheza shoo wake wakiwajibika jukwaani hapo.



Wasanii wanaunda kundi la TIP TOP Connection wakiwa kwenye pozi la pamoja.
Professa Jay (kushoto), akipozi na MwanaFA, nyuma ya jukwaa la Fiesta.


DJ Fetty, B12 na Mchovu wakiwa kwenye pozi nyuma ya jukwaa.
Msanii kutoka THT, Amini Mwinyimkuu, akipagawisha kama Michael Jackson.

Warembo hawa nao hawakuwa nyuma kuonyesha swagger zao.
MwanaFA, akipagawisha.
Ludacris akipagawisha.
Professa Jay, akionyesha uwezo wake jukwaani.
Mashabiki wakipagawa na midundo ya Fiesta.





5 comments:

Anonymous said...

du lina tena sijui unataka nini

Anonymous said...

sifa zinaaza kumpagawisha lina anakokwenda sasa ni kubaya

Anonymous said...

AU NDIO MAMBO YA MAREKANI HAYO YA KUTUALIA UCHI UCHI POLE

Anonymous said...

MSICHANA MZURI KM LINA HATA AKI PARFOM NA KANIKI ATATOKA ILE MBAYA SIO STAIL HIZO UNAZOTULETEA SASA

Anonymous said...

NAKUPENDA LINA NAKUKUBALI ACHANA NA MAMBO YA KUIGA IGA YATAKUSHUSHA SASA HIVI