Social Icons

Friday, October 8, 2010

GEA HABIB SITAKI UKE WENZA NI BORA NIACHIKE!!

Gea Habibu alizaliwa 1981 katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam na kuanza shule ya msingi 1989 katika Shule ya Kurasini Temeke jijini Dar es Salaam na kuhitimu mwaka 1995 ambapo alifanikiwa kujiunga Kidato cha Kwanza kwenye Shule ya Sekondari Jitegemee hadi alipohitimu Kidato cha Sita 1999 kisha kujiunga na Chuo cha Uandishi wa Habari cha Times kilichopo Ilala jijini Dar, kwa muda wa mwaka mmoja.
Hayo ni kwa uchache tu, zaidi ungana nami uweze kujua yale ambayo huenda ulikuwa huyajui kuhusu mwanadada huyu.
TQ:Kwanini uliamua kuwa mtangazaji na si kazi nyingine? Je,kuna aliyekushawishi?
GEA:Hakuna mtu aliyenishawishi kuwa mtangazaji ila mimi mwenyewe nilikuwa napenda sana kusaidia jamii kutokana na hilo njia pekee niliamua kusomea fani hii.
TQ:Ni matatizo gani ambayo umekuwa ukikumbana nayo kupitia fani yako?
GEA:Aah! Kusema kweli kutokana na ugumu wa kazi ya uandishi wa habari matatizo nakutanayo mengi tu ingawa mara nyingi nayachukulia kama changamoto za kazi.
TQ:Wanawake wengi wamekuwa wakikumbwa na skendo ya kutoa rushwa ya ngono ili kufanikisha mambo yao na inadaiwa hata wewe ulipitia njia hiyo kupata kazi yako je, unalizungumzia vipi hilo?
GEA:Kwa upande wangu sijawahi kutoa rushwa ya ngono kwakuwa najiamini,nina uwezo mkubwa wa kufanya kazi. Wanaoitanguliza hiyo bora waiache kwani madhara yake ni makubwa kuliko wanavyofikiri.
TQ:Sawa! Turudi kwenye maisha yako ya kimapenzi najua umeolewa je,unaifurahia ndoa yako?
GEA:Yah! Naifurahia sana ndoa yangu maana naamini mume wangu ananipenda kuliko kitu chochote kile.
TQ: Je, ni kitu gani kinachokuvutia zaidi kwa mumeo?
GEA:Duh! We naye, naweza kusema kila kitu cha mume wangu kinanivutia.
TQ:Katika familia yako umejaaliwa kupata watoto? Na je ungependa kuzaa watoto wangapi?
GEA: Nina watoto wawili hadi sasa na malengo yangu ni kuwa na familia ya watoto watatu tu.
TQ:Najua wewe ni muumini wa dini ya Kiislamu ambayo inaruhusu mume kuwa na mke zaidi ya mmoja, je akitaka kuongeza mke wa pili utakuwa tayari kwa hilo?
GEA: Siku zote kwa hilo siko tayari labda aoe bila taarifa yangu na asiniambie ukweli.
TQ:Unadhani ni kipi kilichomfanya mumeo akuoe wewe na si mwanamke mwingine?
GEA:Naweza kusema ilikuwa imeishapangwa na Mungu anioe mimi.
TQ:Ni jambo gani la huzuni lililokuumiza sana katika maishani yako?
GEA: Siku nilipofiwa na baba yangu mzazi na siku mdogo wangu, mtoto wa mama mdogo aliponifia mikononi mwangu hospitalini. Nikikumbuka matukio hayo mawili hadi leo huwa nakosa raha.
TQ:Nini malengo yako ya baadaye?
GEA: Ni kujiendeleza zaidi katika kazi yangu ya utangazaji.
TQ: Unawashauri nini mastaa wenzako wa kike?
GEA: Wajiheshimu wawapo mbele za watu. Waache majivuno yasiyo na msingi na kwamba wanapopata kazi wafanye kwa bidii bila kusubiri kusukumwa.

TENQUESTION UTAISOMA KUPITIA MATEJA20 KILA SIKU YA IJUMAA.

0 comments: