Monday, January 9, 2012
Wednesday, January 4, 2012
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Moh'akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Umwagiliaji Maji na Mazingira huko kianga Wilaya ya Magharibi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja ikiwa ni shamra shamra za kuadhimisha miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Moh'd Aboud Moh'd akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Umwagiliaji Maji na Mazingira huko kianga Wilaya ya Magharibi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja ikiwa ni shamra shamra za kuadhimisha miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Moh'd Aboud Moh'd akifungua Kizuizi cha Maji kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Umwagiliaji Maji na Mazingira huko kianga Wilaya ya Magharibi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja ikiwa ni shamra shamra za kuadhimisha miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
NUKUU YA LEO
“Gezaulole baba, Gezaulole mama ee,
Twendeni Kibugumo na Mwanadilato kwenye makao mapya,
Gezaulole baba, Geza ulole mama eee!”
Ndugu zangu,
Hapa nanukuu gazeti la Mwananchi leo Jumatano; “Majuzi, Dk Magufuli alifanya ziara ya ghafla katika eneo la vivuko hivyo na kuwaambia wananchi waliomzomea kwamba kama wakishindwa kulipa nauli hiyo ya Sh200 ni vyema wakapiga mbizi baharini au kuzunguka Kongowe kuingia katikati ya jiji au warudi vijijini wakalime.”- Mwisho wa kunukuu.
Utotoni katika Dar es Salaam hii, nilishuhudia kwa macho yangu msako wa wazururaji. Niliona jinsi mgambo wa jiji walivyokuwa wakiwadhalilisha vijana na watu wazima kwa kuwakamata, kuwafunga mashati na kuwapandisha kwenye malori tayari kwa safari za kwenda Gezaulole. Kosa lao, walikuwa wakizurura mijini bila kazi. Hivi, anayetafuta kazi atabaki nyumbani kuisubiri, si ni lazima apige mguu kuitafuta? Sijui leo ungefanyika msako wa wazururaji Dar yangehitajika malori mangapi?
Na miaka ile ya sabini tulipokuwa watoto tulisikia hata nyimbo za redioni kuhimiza ‘ wazururaji’ waende kwenye vijiji vipya vilivyoandaliwa na Serikali kama makazi ya ‘ Wazururaji’. Watoto wa enzi hizo huenda tunakumbuka wimbo huu;
“ Gezaulole baba, Gezaulole mama ee,
Twendeni Kibugumo na Mwanadilato kwenye makao mapya,
Gezaulole baba, Geza ulole mama eee!”
Kigamboni ya enzi hizo ilikuwa shamba kweli. Wengi wa waliofikishwa huko Gezaulole na vijiji vingine kule Kigamboni wakayaanza maisha mapya ya vijijini. Kuna waliokimbia Gezaulole wakarudi tena mjini au kwenye vijiji vyao vya asili. Kuna waliobaki huko Gezaulole, wakafyeka mapori yao. Wakaanza kilimo, . Wakaizoea hali mpya. Wakajenga familia zao huko.
Ajabu, leo wenye fedha ndio wanaokwenda kuyanunua kwa bei ya hadaa, maeneo ya watoto na wajukuu wa ‘ wazururaji’ wa enzi za Mwalimu. Kuna watoto na wajukuu wa ‘wazururaji’ waliobaki na vieneo vidogo. Miongoni mwao ndio hao wanaofanya shughuli za kusukuma mikokoteni na kuendesha maguta.
Ndio hao, waliokisikia kilio cha kutaka uwepo wa pantoni ya uhakika kwa miaka nenda , miaka rudi. Wamesikia kilio cha kujengewa daraja pia na ahadi zake. Na sasa wanaongezewa nauli ya kivuko kwenda na kurudi mjini.
Ni hivi; mkazi wa Magomeni hata kama hana nauli anaweza kutembea kwa miguu kukatisha Jangwani na akamwona mgonjwa wake Muhimbili, au kwenda kuhangaikia kibarua Kariakoo. Na jioni ikifika, hata kama hana nauli ya Daladala, atakatisha Jangwani na kufika Magomeni kwenye chumba chake cha kupanga.
Lakini, mkazi wa Kigamboni kama hana nauli ya mia tatu ya pantoni na kama anataka kuvuka kwenda kumwona mgonjwa wake Muhimbili au kuhangaikia kibarua Kariakoo ana mawili, kwa mujibu wa Magufuli; ama apige mbizi au azungukie Kongowe, kwa miguu, mwendo wa nusu siku kama si siku nzima. Na hapa ndipo ilipo hoja ya msingi ya kumfikiria mtu wa kawaida wa Kigamboni, Gezaulole na kwingineko ng’ambo ya pili ya bahari.
Vinginevyo, kwa kusema kuwa asiye na nauli arudi kijijini akalime ina maana pia, kuwa kuishi Jangwani, Mburahati na Mabibo kunaweza kuwa na nafuu zaidi kwa mtu wa Kigamboni mwenye hali ngumu kiuchumi. Kwamba hatimaye tunawaambia watoto na wajukuu wa ‘ wazururaji’ wa enzi za Mwalimu; “Rudini mjini’. Na wimbo ule leo labda ungeimbwa hivi;
“ Mburahati mama, Mburahati baba ee,
Rudini Jangwani, na Mwananyamala kwenye maisha bora!”
Haki ya Mungu!
Maggid Mjengwa,
Msamvu, Morogoro.
NI SHUGHULI PEVU BONGO MOVIES
MBUNGE WA WAWI (CAFU), HAMAD RASHID ATIMLIWA KAZI
Monday, January 2, 2012
UZINDUZI WA DAR LIVE NI HISTORIA MPYA MBAGALAka Mambo haya yametokea katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala usiku wa kuamkia leo.
Inspector Haroun akiongoza Gangwe Mobb kupagawisha mashabiki.
Profesa J: Nikisema Dar, Sema Live!!!
…Jay akiongea na mashabiki wake.
……akiwajibika na mdogo wake..
....show girls wa Mbagala...full mzuka!
...totozi za Mbagala kama mamtoni!
Mzee Yusuf alikoleza moto wa Dar Live.
Leila Rashid wa Jahaz Modern Taarab akiwadatisha mashabiki.
Juma Nature na wanaume halisi wakikoleza moto wa maraha.
Wanenguaji wa Extra Bongo wakiongeza utamu wa uzinduzi huo.
Mshereheshaji wa onyesho hilo kutoka Times Fm akifurahi na mashabiki.
Kundi la Wanaume Halisi linaloongozwa na Juma Nature likinyanyuliwa juu ya jukwaa.
Mwanamuziki wa kundi la Wanaume Halisi, ajulikanaye kama KR (kushoto) akiwa na mtoto wa mpigapicha wa Global, Ajibu Issa Mnally.
Baadhi ya wasanii waliotoa burudani jana.
Samaki na Nyama choma za kufa mtu zilikuwepo...
DAR LIVE, ukumbi wa kisasa wa maraha ya kila aina ulioko Mbagala Zakhem, Dar es Salaam, jana ulizinduliwa rasmi na kufurika watu lukuki waliojimwaya katika starehe za muziki, vinywaji, kuogelea, kufaidi mabembea, na kadhalika. Miongoni mwa starehe za kuvunja mipini ya shoka zilizopatikana katika kituo hicho, ni muziki ulioangushwa na Jahazi Modern Taarab, Extra Bongo na wasanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Profesa Jay, Gangwe Mobb na Wanaume Halisi wakiongozwa na Juma.
Sunday, January 1, 2012
UZINDUZI WA DAR LIVE ULIANZA KWA SHANGWE
Watoto wakiwa katika mabembea.
Michezo ya baiskeli ilikuwa kivutio kikubwa kwa watoto.
UKUMBI wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam umezinduliwa leo saa nne na kuwavutia watu wengi wa eneo hilo na vitongoji vyake ambapo kwa ajili ya kupata burudani ya mwaka mpya iliyojumuisha kila aina ya ‘maraha’ ikiwa ni pamoja na michezo ya watoto kwa watu ambao waliamua kujimwaga hapo na familia zao.
Mabembea ya ‘mzunguko’ yaliwavutia watoto kinoma.
Waliotaka kupanda ‘ndege’ walipata fursa hiyo.
Mratibu wa burudani katika kituo hicho, Juma Mbizo (mwenye kofia), akiwa na familia yake.
Baadhi ya watoto wakiingia katika kituo hicho.
Hapa ni moja ya vivutio vya ukumbi huo.
TAMASHA LA BONGO 50 LILIVYOFANA SIKU YA MKESHA WA MWAKA MPYA 2012
PROFESA KAIJAGE ASHEHEREKEA
KUTIMIZA MIAKA 70
Mmoja ya wajukuu aliyewawakilisha wenzake akimlisha keki babu yake. Mmoja ya wajukuu aliyewawakilisha wenzake akimlisha keki bibi yake. Profesa Fredy Kaijage akiwakaribisha nyumbani kwake Waziri wa Ulinzi na JKT Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na mkewe na mwanae ambao nao walihudhuria sherehe ya kuadhimisha miaka 70.
Wageni wakijaribu kubadilshana mawazo. ...pongezi zilikuwa zikimiminika kwa Profesa Fredy Kaijage kutoka kwa marafiki. ...Mwanangu hujambo???? Mbona sikuhizi hauji tena nyumbani kusalimia. Binti anajibu; baba mambo yamekuwa mengi, nisamehe bure. Hapa napo palinoga sana...Maprofesa walikutana kila mmoja alikuwa na lake...basi raha tu.. Mjadala huo ulikuwa ukiongozwa na Profesa Samwel Wangwe (mwenye miwani). Profesa Fredy Kaijage akiongoza wageni wake kupakua chakula. Profesa Fredy Kaijage, akiongeza nguvu kwa kupata chakula. Mijadala ya hapa na pale iliendelea ...Dah! kumbe ndizi nimezipita...sasa pakua nyingi ili tukale wote. Hahahahahaha ndivyo alivyokuwa nakazia ... Profesa Samwel Wangwe (kushoto) nae hakuwa nyuma Mtoto mkuwa wa Profesa Kaijage akiwa pamoja na watoto wake na wa kaka zake Furaha zilitawala Wajukuu wa Profesa Kaijage hawakuwa nyuma kwenye suala la chakula Profesa Kaijage (wa kwanza kulia), Mkwe Theresa (wa kwanza kushoto) na mwanae wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi na JKT Dkt. Hussein Mwinyi akiwa na mkewe. Profesa Kaijage na familia yake wakiwa katika pichaya pamoja na Waziri wa Ulinzi na JKT Dkt. Hussein Mwinyi na mkewe. ...Wala hata Ruge Mutahaba hakukosa nae
Muda wa kuserebuka uliwadiaaaaaaaaaaa
Wajukuu wakitoa salamu zao kwa babu yao Wakitoa zawadi yao Profesa Samwel Wangwe akitoa salamu zake. Familia pamoja Baba na mwana wakijiachia mara baada ya kuupokea mwaka mpya 2012 pongezi ziliendelea Kumbukumbu ya mwaka 2012