Mh Cheyo, Mh Balozi Kallaghe na Frank wakibadilishana mawazo
Picha ya Pamoja Mh Balozi na Mh Cheyo
Salam,
Urban Pulse Creative walipata fursa ya kukutana na Mbunge wa Bariadi mashariki Mh John Mamose Cheyo katika Ubalozi wetu wa Tanzania mjini London hapa nchini Uingereza alipokuja kukutana na Mh Balozi Peter Kallaghe. Vilevile Baraka Baraka kutoka Urban Pulse alifanya nae mahojiano maalum na kujadili mambo kadhaa kama dhumuni ya ziara yake, mchakato wa Katiba mpya, miaka 50 ya uhuru wa Tanzania na mipango ya maendeleo katika jimbo lake na mengineyo
Mahojiano hayo yatarushwa hivi karibuni, usikose kuangalia
Asanteni,
URBAN PULSE CREATIVE
0 comments:
Post a Comment