UGANDA YATWAA KOMBE LA TUSKER CHALLENGE CUP 2011
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dk. Ali Mohamed Shein akikabidhi kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 kwa wachezaji wa timu ya Uganda (The Cranes) mara baada ya timu hiyo kushinda kombe hilo kwa kuifunga timu ya Rwanda (Amavubi) katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii jijini Dar es salaam.
Ilikuwa ni fainali ya kuvutia kwa timu zote mbili kutokana na kiwango kilichoonyeshwa katika dakika 90, timu hizo zilitoka suluhu ya magoli 2-2 ambapo dakika 30 ziliongezwa lakini hazikuzaa matunda kwa timu zote mbili, mpaka ilipofika wakati wa mikwaju ya penati, timu ya Uganda ilipata penati 4-3 dhidi ya Rwanda, hivyo Uganda kutawazwa mabingwa wapya wa kombe hilo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dk. Ali Mohamed Shein akimpongeza mmoja wa wachezaji wa timu ya Uganda baada ya timu hiyo kuwa mabingwa wapya wa TUSKER CHALLENGE CUP 2011.
Wachezaji wa Rwanda wakiwa haamini kilichotokea mara baada ya mpira kumalizika kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo.
Kutoka kulia ni Carol, Moureen na Bahati kutoka R&R wakiwa na baadhi ya warembo wakifurahi baada ya kumaliza kazi.
Wadau kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti na R&R wakifurahia kumalizika kwa kazi ya mashindano hayo kwa mafanikio.
Katikati ni Richard Wells Mkurugenzi wa kampuni ya bia ya Serengeti akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo Ephraim Mafuru na Moses Kebba Meneja Masoko wa Tusker Lager.
Zawadi zikiandaliwa kulia ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya bia ya Serengeti na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo Ephraim Mafuru.
Wachezaji wa Uganda kulia na Rwanda wakichuana vikali kuwania mpira wakati timu hizo zilipokutana katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment