Social Icons

Friday, December 9, 2011

RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AONGOZA WATANZANIA KUADHIMISHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA

Rais Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na viongozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania, yanayoendelea kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam mchana huu hapa akisalimiana na Rais wa Namibia Mh shimiwa Hifikepunye Pohamba.

Rais Jakaya Kikwete akielekea Jukwaa kuu mara baada ya kukagua gwaride katika sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania kwenye Uwanja wa Uhuru, akiwa ameongoza na Mkuu wa Majeshi nchini Jenerari Davis Mwamunyange.
Rais Jakaya Kikwete akikagua Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania kikosi hiki ni cha Jeshi la Wananchi.
Rais Jakaya Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania kikosi hiki ni cha Jeshi la Wananchi wanaume.
Rais jakaya Kikwete akipokea heshima wakati mizinga ikipigwa na jeshi la wananchi kwa heshima ya Rais.
Hiki ni kikosi cha Jeshi la wananchi wanamaji kikiwa tayari kutoa heshima kwa amiri jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tamnzania Dk. Jakaya Kikwete.
Rais Dk. Jakaya Kikwete akipungia mkono wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya kuongoza sherehe za miaka 50 ya Tanzania.
Msafara wa Rais Dk Jakaya Kikwete ukiwasili kwenye uwanja wa Uhuru tayari kwa kuongoza watanzania katika sherehe za miaka 50 ya Tanzania.
Walinzi wa rais walikuwa kivutio katika sherehe.wakati msafara wa Rais Dk. Jakaya Kikwete ukiwasili katika uwanja wa Uhuru leo.
PICHA: FULL SHANGWE BLOG

0 comments: