Social Icons

Wednesday, December 21, 2011

MAFURIKO YACHAFUA HALI YA HEWA MIKOCHENI Maji yakiwa yamelizingira jengo laMayfair Plaza.


KUFUATIA mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es Salaam, maeneo ya Mikocheni (A), yameathirika vibaya baada ya kukumbwa na mafuriko na kusababisha adha kubwa kwa wakazi wake.

Baadhi ya maeneo yaliyoathirika zaidi ni katika Hospitali ya (TMJ), jengo la Shoppers Plaza, Mayfair na Tanesco.


Jengo la hospitali ya TMJ likiwa limezingilwa na maji.


Mtoto akikwea ukuta kujisalimisha.


Baadhi ya wafanya biashara wa vocha katika eneo la Mayfair Plaza wakiwa juu ya vibanda vyao.


Wasamaria wema wakitoa msaada kusukuma gari baada ya kuzimikia kwenye maji.

Lango kuu la kuingia ofisi za Tanesco Mikocheni likiwa limezingirwa maji.


Ukuta wa jengo la Tanesco ukiwa umezingirwa maji.


Nyumba ikiwa imejaa maji.

Vijana wakisubiri maji yapunguwe waweze kupita.


Barabara ya kuelekea kwenye nyumba ya Mwalimu Julius Nyerere ikiwa imejaa maji.



0 comments: