UZINDUZI wa ukumbi wa Dar Live, Mbagala jijini Dar es Salaam unaotarajiwa kufanyika Januari Mosi, 2012 ndiyo ishu inayogonga kwenye vichwa vya wengi kwa sasa ambapo wasanii kibao wakiongozwa na Juma Kassim Kiroboto ‘Nature’ wataangusha bonge la shoo.
Wasanii wengine, Haroun Kahena ‘Inspekta’ na Karama Bakari ‘Luteni Kalama’ wanaounda Gangwe Mob nao watakamua jukwaa moja na Kundi la Jahazi Modern Taarab bila kuwasahau Extra Bongo.
“Mwaka Mpya ndiyo siku ambayo Wabongo watajionea wenyewe maujanja yanayopatikana ndani ya Dar Live! Mbagala hivi sasa kumekuwa kwa kishua, hii siyo ya kukosa watu wangu,” alisema Nature.
0 comments:
Post a Comment