NAPE ALAMBA SHAHADA YA PILI YA UONGOZI


Watangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Chanel Ten Fredy Mwanjala, Salama Hamadi na Zainab Abdul, wakimpa zawadi ya hongera, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye ametunukiwa shahada ya pili ya uongozi kwenye mahafali ya kumi ya Chuo Kikuu Mzumbe, kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Nape akipongezwa na baba yake mdogo, Mzee Galus Abeid katika mahafali hayo. Katikati ni mama wa Nape, Kezia Alfred.

Nape akipongezana na mhitimu mwenzake kwenye mahafali hayo, Wilfred Gallaba ambaye ni Mkaguzi wa hesabu Ofisi ya Ukaguzi ya Taifa.

Nape (kushoto kwenye kona) akiwa na wahitimi wenzake wakati wakinutunukiwa sahada ya pili ya uongozi kwenye mahafali hayo.
0 comments:
Post a Comment