Social Icons

Wednesday, November 9, 2011

SAUDA MWILIMA AVISHWA PETE YA SHILINGI MILIONI 3Sauda Mwilima (kulia), akivishwa pete na mchumba wake Kauli Juma a.k.a Best Friend ndani ya ukumbi wa Star Coco Beach.

MTANGAZAJI wa kituo cha Star Tv, Sauda Mwilima hatimaye amechumbiwa na kuvishwa pete ya thamani ya shilingi milioni 3 na jamaa mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Kauli Juma ‘Best Friend’ Mateja20, ina full data.

Tukio la kuvishwa pete kwa mtangazaji huyo lilifanyika katika Ukumbi Coco star Masaki jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mastaa mbalimbali wa Bongo wakiwemo ndugu na jamaa wa karibu wa mtangazaji huyo.

Tukio la kuvishana pete lilifanyika majira ya saa 12:30 usiku baada ya kumaliza zoezi la ufunguzi wa shampeni iliyokuwa imeaandaliwa kama changa la macho kwa wangeni waalikwa ambapo wengi wao walitinga ukumbini hapo wakiamini wanaeenda kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake.

Mshereheshaji wa shughuli hiyo ambaye ni msanii wa filamu Bongo, Christina Manongi ‘Sintah’ alianza kwa kuwaomba radhi waalikwa kwa uongo uliyotumika na hatimaye aliitwa mchumba wa Sauda Best Friend tayari kwa kukamilisha zoezi hilo.

Kabla hajanyanyua mkono wa Sauda tayari kwa kuweka pete hiyo ghafla alitokea Babu yake na Sauda aitwaye Zahoro Selema na kupinga kuvikwa pete hiyo bila kupewa chochote ambapo Best Friend alimlegeza Babu kwa kumpa shilingi elfu 15 na kujikuta akiruhusu tukio hilo kufanyika.

Mastaa waliohudhulia katika hafla hiyo ni Jacqueline Wolper, Wema Sepetu, Maimartha Jesse, Miradi Ayo, Janeth Mwenda, Steve Nyerere, Juma Chikoka, Husna Mauld ‘Sajenti’ Taji Rihundi na wafanyakazi wenzake wa staa TV.

Sherehe hizo pia zilitumbuizwa na wasnii kibao wa muziki wa kizazi kipya kama Linex, Q Chief, Mrisho Mpoto na Naseeb Abdul ‘Diamond’ hawa wote pia walimpongeza Sauda kwa kufikia hatua hiyo na kumuomba awe mvumilivu ili wafikie kwenye hatua ya kufunga pingu za maisha.
































1 comments:

Unknown said...

HATUA ALIOFIKIA SAUDA NA MSHIKAJI WAKE NI NZURI CHA MSINGI NI UVUMILIVU.2 HAO MASTAA WETU HAPA BONGO HAWEZI KUVAA NGUO ZA KUJISTIRI JAMANI HEBU UFIKE MDA WAJARIBU KUJIHESHIMU KTK MAVAZI