JACK : TIMBULO NDIYE NILIYECHAGUA KUWA NAYE WAKATI HUU!
Msanii wa filamu Bongo Jacqueline Pentezel a.k.a Jack wa Chuzi, juzikati aliweka wazi kuwa kwa sasa ndiyo muda muafaka kwake kumpa penzi chipukizi wa Bongo Fleva Ally Timbulo, anayetikisa jiji na wimbo wa " Domo langu zito".
Akizungumza na MATEJA20, juzi alisema kuwa kwa sasa hahitaji ushauri wowte kutoka kwa mtu kwani kuwa na Timbulo ameamua mwenyewe na hakuna mtu atakye mpangia mwanaume wa kuwa naye kwenye maisha haya.
Jack ambaye aliweka wazi uhusiano wake na bwana mdogo huyo kupitia magazeti ya Global Publishers LTD, anasema "Kila kukicha nimekuwa nikiulizwa maswali mengi sana kutoka kwa wadau wa burudani hii juu ya Timbulo jambo ambalo mwenyewe linanishangaza na kushindwa kuelewa nia yao hasa nini kwani mwenyewe naona Timbulo ndiye mwanamue halisi wa kuwa naye,"
"Kwakutaka kuonyesha msimamo wangu sasa naomba watu wote wasihangaike kuuliza maswali mengi kwani naamini Tibulo ni mwanaume halisi na nitakuwanaye siku zote za maisha yangu wala hakuna mtu atakaye nibadilisha uamuzi huu,"
"Nanaomba wafahamu kuwa Timbulo ananipenda sana na ndiyo maana kuna wimbo ambao tayari ameshauachia na umeniimba mimi wimbo huo unatambulika kwa jina la Waleo Wakesho," alisema Jack ambaye kwa sasa anapika na kupakua nyumba moja na Timbulo.
0 comments:
Post a Comment