Social Icons

Tuesday, November 22, 2011

CHEKI VIDEO YA UWOYA KUOMBA MSAMAHA KWA MUMEWE!

Na Waandishi Wetu
ALICHOKIUNGANISHA Mungu, mwanadamu hawezi kukitenganisha! Hatimaye lile muvi la mwaka lililochukua nafasi wiki iliyopita la kuvunjika kwa ndoa ya Irene Pancras Uwoya na Hamad Ndikumana ‘Kataut’, limemalizika kwa uzuri, wapendanao hao wamerudiana, The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda limeshiriki kwenye mchakato huo ‘eituzedi’.

HALI ILIKUWAJE?
Baada ya Uwoya kutangaza kuachana na mumewe waliyedumu kwa takribani siku 822 na habari hiyo kutikisa mtaani, sistaduu huyo mkali wa filamu za Kibongo alimtafuta mumewe ili wayamalize, lakini jamaa akamtolea nje.

NDIKUMANA ANAFUNGUKA
Saa 4:00 asubuhi ya Alhamisi, nyumbani kwa wazazi wa Uwoya maeneo ya Mbezi Jogoo, Dar, Ijumaa Wikienda lilijaa tele ambapo lilipokelewa na Ndikumana aliyefika kumjulia hali mama mkwe wake kwa kuwa alikuwa mgojwa kwa siku tatu.

Ndikumana alifunguka: “Ni kweli nilikuwa sipokei simu ya mke wangu (Uwoya) kwa sababu alinidhalilisha sana kusema hakuwahi kunipenda.

“Nilimpa sharti la kuwaomba msamaha wazazi wake na wakimsamehe, mimi sina tatizo naye.
“Kweli mke wangu amefanya hivyo kwa watu wote na anajutia kwa kauli yake hiyo.
“Natamka kutoka moyoni mwangu, sina kitu rohoni na nimemsamehe mke wangu.

MAISHA LAZIMA YAENDELEE
Katika mahojiano na Ijumaa Wikienda, Ndikumana alisema kuwa kutokana na mambo yote yaliyotokea, lazima maisha yaendelee hivyo watu waiombee ndoa yao iwe imara zaidi.

HATIMAYE WASHIRIKI JOTO LA WANANDOA
Wakati hayo yakiendelea, kazi ya Ijumaa Wikienda ilikuwa ni kutoa somo la namna ya kuvumiliana kwenye ndoa huku wahusika wakiipokea elimu hiyo kwa mikono miwili.

Hata hivyo, baada ya somo kuwakolea, wanandoa hao waliojaliwa mtoto mmoja wa kiume, Krish walisogeleana, wakatazamana usoni wakilengwalengwa na machozi ya furaha.

Katika kuonesha kila mmoja ‘alimisi’ joto la ndoa kutoka kwa mwenzake, Uwoya na Ndikumana walikumbatiana kimahaba na kubusiana. Kila mmoja alionekana kuwa na ‘ukame’ na mwenzake.

UWOYA AJUTA TENA MBELE YA MUMEWE
Neno najuta…najuta…najuta, lilikuwa halikauki kinywaji mwa Uwoya, alimwambia tena mumewe mbele ya Ijumaa Wikienda: “Mume wangu najuta, ilikuwa ni hasira tu, naahidi sitarudia tena na nakupenda sana Hamad (Ndikumana).”

NINI KITAFUATA?
Baada ya kukubaliana kurejesha heshima ya ndoa, Ijumaa Wikienda lilitaka kujua mipango ya maisha yao itakavyokuwa ambapo Ndikumana, huku akiwa ameshikilia kiuno ‘babkubwa’ cha Uwoya alisema:
“Tupo hapa kwa mama kwanza tunamlea mtoto wetu na wazazi wanataka tukae hapa kwa muda ili waangalie mienendo yetu.”

UWOYA AHOFIA IJUMAA WIKIENDA LIKING’OA NANGA MAMBO YATAKUWA MABAYA
Katika hali ya kushangaza, wakati timu ya Ijumaa Wikienda ikitaka kung’oa nanga kurejea ofisini, Uwoya aliomba Ndikumana aulizwe tena kama kweli waandishi wakiondoka hali haitakuwa mbaya.
Ndikumana: (Huku akicheka na kumbusu Uwoya) Sina kinyongo moyoni mwangu, nimemsamehe saba mara sabini.”

NENO LA IJUMAA WIKIENDA
Sala, dua na jitihada zetu za kutaka wawili hao warudiane zimefanikiwa kurejesha amani na matumaini yaliyopotea katika ndoa ya dada yetu na mwanasoka huyo wa Rwanda. Tunawatakia kila la heri- Mhariri.

0 comments: