KATIKA hali isiyotazamiwa na wengi, Bendi ya Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic Modern Taarab, zinatarajiwa kuvaana katika jukwaa moja Jumapili hii 30/10/2011 katika Ukumbi wa Traver tine Hotel – Magomeni jijini Dar es Salaam.
Mashauzi Classic inayoongozwa na Isha Ramadhan maarufu kama Isha Mashauzi imekuwa ikichukuliwa kama ndiyo bendi mkuu pinzani ya wa Jahazi tangu iundwe rasmi miezi michache iliyopita.
Isha ambaye kabla ya kuunda bendi ya Mashauzi aliitumikia Jahazi iliyo chini ya Mfalme Mzee Yusuf na kujizolea umaarufu mkubwa kupitia nyimbo za “Hayanifiki” na “Ya wenzenu Midomoni”.
Kwa jinsi Isha alivyoondoka bendi ya Jahazi bila kuaga imekuwa ikiaminika miongoni mwa watu wengi kuwa yeye na Mzee Yussuf ni kama paka na panya na hivyo kupelekea onyesho hilo kuteka hisia za wapenzi lukuki wa taarab.
Isha Ramadhan amedhamiria kulitumia onyesho hilo kama sehemu rasmi ya kumuaga Mzee Yussuf na kumshukuru kwa kumjenga hadi kumfikisha hapo alipo.
Katika kunogesha zaidi onyesho hilo liliopewa jina la “Usiku wa Baba na Mwana”, Tanzania One Theatre chini ya Kapeteni Komba (Mh) imetoa jukwaa kubwa kabisa litakalowawezesha watu kushuhudia onyesho hilo bila adha yoyote.
0 comments:
Post a Comment