DIVA: WABONGO WANAPENDA KULAZIMISHA PENZI
Na Erick Evarist
MSHIKA 'mic' kunako redio ya Clouds Fm, ‘Diva’ amefunguka kuwa, wabongo wengi wanapenda kulazimisha penzi hata wakati linapokuwa limekwisha.
Akichezesha taya na paparazi wa Mateja20 kwa njia ya simu hivi karibuni Diva alidai kuwa kamwe yeye huwa mapenzi hayamsumbui kwa kuwa hayajali kiivyo kama wengine yanavyowatesa alisema hata ikimtokea mpenzi wake wamezinguana basi huwa haimsumbui kiivyo.
‘‘Kwanza mimi sijawahi kuteswa na mapenzi sababu huwa siyajali na hata ikitokea tumefikia hali ya kutoelewana basi ni kuchukuwa time na maisha yanaendelea kama kawa,”
‘‘ Tatizo watu wengi huwa wanapenda kubembeleza sana wakati wanajua kabisa penzi likiisha huwa limeisha wala halihitaji kubembelezana,’’ alisema Diva.
3 comments:
usimayo ni yakweli kabisa wabongo wanapenda sana kulazimisha penzi humuoni wema amekataliwa na Diamond matokeo yake analazimisha lazima awe naye hebu fikiria nini hapo kitatokea? mtu akikwambia basi ujuwe ni basi usitake kulazimisha hakuna mapenzi hapo
longa longa waambie hao!!!!!!!!!!!!!
WEMA UMESIKIA HIYOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Post a Comment