JAN POULSEN AVUTA MASHINE 22 ZA KUIANGAMIZA WA CHAD- N'DJAMENA
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen leo ametangaza kikosi cha wachezaji 22 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa Novemba 11 mwaka huu jijini N’Djamena.
Mchezaji aliyeitwa kwa mara ya kwanza ni kipa Mwandini Ally wa Azam huku pia akimjumuisha kwenye kikosi chake mshambuliaji wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), Thomas Ulimwengu.
Kikosi kamili ni makipa Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya), Erasto Nyoni (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Godfrey Taita (Yanga) na Juma Jabu (Simba).
Viungo ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Ramadhan Chombo (Azam) na Shomari Kapombe (Simba).
Washambuliaji katika kikosi hicho ni Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden), Hussein Javu (Mtibwa Sugar) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).
Timu hiyo inatarajia kuingia kambini, Novemba 3, mwaka huu jijini Dar es Salaam, na pia inatarajia kuondoka nchini Novemba 9, kulelekea N'Djamena kwa ajili ya mechi hiyo. Stars na Chad zinatarajia kurudiana tena Novemba 15, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari- (TFF)
0 comments:
Post a Comment