Social Icons

Wednesday, October 26, 2011

CHEKI MATUKIO YA AJALI KATIKA BASI LA DELUX KIBAHA

Moja ya maiti ambazo ziliteketea kwa moto kufuatia ajali ya basi la Delux Coach lilopata ajali ya kupasuka gurudumu la mbele maeneo ya Misugusugu Wilayni Kibaha mkoani Pwani Oktoba 25,2011na kupinduka kabla ya kuwaka moto na kupoteza maisha ya abiria wa basi hilo takribani 25 na wengine zaidi ya 17 kujeruhiwa vibaya. Basi hilo lilikuwa linatokea jijini Dar es Salaam likielekea Dodoma.
Mkuu wa Mokoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza akizungumza alipofika eneo la tukio.
Wananchi na polisi wakiangalia mabaki ya basi hilo baada ya kuteketea kabisa kwa moto.
Mmoja wa watu waliokuwa wakitoa mabaki ya miili ya watu walioteketea kwa moto akiendelea na zoezi la kuangalia iwapo kama kuna masalia yeyote.
Basi liliteketeakabisa na mabaki ya miili ya watu ililazimu kukusanywa kwa beleshi.
Maiti zilikuwa ni nyingi na hata utambuzi wake ulikuwa mgumu.


Wananchi wa Kibaha wakiangalia ajali hiyo.
Blogu hii inaungana na watanzania wote kuwaombea heri waliofikwa na msiba huu mkubwa na Mungu azihifadhi mahala pema roho za marehemu wote.

(Picha zote na Yassin Nicas Mtei wa Father Kidevu Blog-Mlandizi)

PICHA: FK BLOG

0 comments: