Majaji wa shindano la Jenga nchi yako, wakifuatilia kwa makini namna wasanii wanavyoonyesha uwezo wao, anayeongea wa pili kutoka kulia ni mmiliki wa studio ya Tattoo Record Bw. Faraja Kiobya, akiwa na majaji wenzake Steven Joseph 'Jobiso' (wa kwanza kulia), na Deogratius Manegella 'Dessamo' (kushoto), anaemfuatia ni Annaclara Aidan 'ACM', mchujo huo unaendelea kufanyika ndani ya Ukumbi wa The Atriums Hotel iliyopo Sinza Afrikasana jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa washiriki wa shindano hilo Sianah Jordan (kushoto), akionyesha uwezo wake mbele ya majaji.
Sianah, akiimba kwa hisia kali.
Mshiriki wa shindano hilo Ramadhan Rajab Jumbe (kushoto), akimimina 'song' zake kwa majaji hao.
Ramadhan akitetea nafasi yake.
Mshiriki wa shindano la Jenga Nchi yako Steven James (kulia), akiwajibika mbele ya majaji katika hotel ya The Atriums Sinza afrikasana jijini Dar, leo hii.Usaili huo ulianza tangu jana ndani ya Hoteli ya The Atriums Sinza Afrikasana jijini Dar es Salaam, ambapo washiriki hao walionesha vipaji halisi na kusababisha usili huo kuwa wakiushindani zaidi kwa kila mmoja kuwania nafasi ya ushindi.
Akizungumza na MATEJA20 Mratibu wa kinyanga’anyiro hicho, Richard Mathew Manyota ambaye pia ni Balozi wa Amani na Ulinzi Shirikishi Tanzania alisema, kwa sasa shindano
“kwa sasa mambo yanazidi kuwa mazuri kani hatua hii inaashilia matokeo mazuri na lengo letu la kuinua vijana wenye vipaji vya kuimba litatimia” alisema Manyota.

0 comments:
Post a Comment