KAMPUNI ya Dimod Integrated Solution & Awareness, imeandaa bonge latamasha na semina ya vijana yenye kauli mbiu: ‘Kwaheri Umaskini, Tujikomboe Tusherehekee miaka 50 ya uhuru kwa pamoja.
Kwa mujibu wa mratibu wa semina hiyo, Mahmoud Omar, ishu hiyo itafanyika katika Viwaja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama, Dar es Salaam kuanzia Septemba 29 hadi Desemba Mosi, mwaka huu.
Alisema lengo la semina hiyo ni kuwainua wajasiriamali wote nchini.
Alisema: “Watakaohudhuria watapata fursa ya kujifunza kutengeneza sabuni za miche na maji, shampoo, mishumaa, mafuta ya kujipaka, lotion, maji ya battery, tomato source, chilli source, unga wa lishe, wine aina zote, biskuti, keki, juice aina zote, ufugaji na kutengeneza vyakula vya mifugo na biashara kwa jumla.”
Alisema ada ya masomo yote itakuwa TSh. 10,000/= kwa masomo ya nadharia na vitendo ambapo itaanza saa 3:00 asubuhi hadi 6: 00 mchana kisha mafunzo yataendelea saa 8: 00 alasiri hadi 12: 00 jioni.
Semina hiyo imedhaminiwa na Global Publishers, wachapishaji wa Magazeti ya Ijumaa, Uwazi, Ijumaa Wikienda, Risasi, Amani na Championi yatakayouzwa mahali hapo.
0 comments:
Post a Comment