LULU ACHAFUA HALI YA HEWA 'BIRTHDAY' YA SHILOLE
Msanii wa filamu Bongo, Zuwena Mohamed 'Shilole' (katikati), usiku wa kuamkia leo alisherekea sikukuu ya kuzaliwa kwake, ndani ya Ukumbi wa Lamada Hotel Ilala jijini Dar es Salaam, ambapo sherehe hiyo ilihudhuriwa na mastaa wenzake wa filamu na marafiki zake kutoka sehem mbalimbali Bongo.
Shilole (kushoto), akimlisha keki msanii mwenzake Jennifer Mwaipaja 'Shumileta' mara baada ya kukata keki hiyo.
Msanii mkongwe wa filamu Bongo, Jacob Steven 'JB', akimkumbatia kwa furaha Shilole muda mfupi baada ya kuingia ukumbini hapo.
Badra (katikati), akimzawadia Shilole baada ya muda wa kutoa zawadi kuwadia.
Msanii wa filamu Daudi, akihangaika kutoa utepe wa Shampeni tayari kwa kuifungua.
Mmoja wa waalikwa wa shughuli hiyo, akibanjuka kwa raha zake baada ya kukolezwa na kinywaji kilichokuwa kikimiminishwa mahali hapo.
Badra akionyesha uwezo wa kucheza katumba mahali hapo.
Waalikwa wakifuatilia mchakato mzima huku wakishushia vinywaji.
Warembo wakibanjuka kwa raha zao katika sherehe hiyo.









Msanii wa filamu Elizabeth Michael 'Lulu' (kushoto), akikisi na mmoja wa waingizaji wa Komedi Bongo, mara baada ya kuponi yake kumtaka kufanya hivyo kwa sharti kama asingeweza kumbusu jamaa huyo basi alitakiwa atoe kiasi cha shilingi 10,000 kama faini ya kuponi hiyo.
Lulu akiwa chini na mshikaji huyo baada ya kupiga kisi.
Lulu akijuta baada ya kufanya upuuzi huo namna hii "mama yangu kumbe paparazi wap!!!"
... baada ya vimbwanga hivyo alikimbilia kufungua shampeni.
Shilole na Sajenti wakiwa kwenye pozi la kusubiria shampeni hiyo.
Catty (kulia), nae alijumuika kusubiria kinywaji hicho.
Sajenti akihamisha keki hiyo baada ya kumwagikiwa na pombe aina ya Amarula kwa bahati mbaya kabla ya kuikata.
Msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel (kulia), akilishwa keki na Shilole mahali hapo.
Msanii wa filamu Mayasa Mrisho (wa kwanza), akiwa katika sherehe hiyo.
Msanii wa kundi la Bongo Dar es Salaam Kulwa Kikumba (kushoto), akiwa katika pozi na Badra (mbele), na msanii mwenzao ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja.
Jini Kabula (kulia), akiwa katika pozi na ... mahali hapo.
0 comments:
Post a Comment