Social Icons

Thursday, September 8, 2011

AIRTEL YAZIDI KUPANUA MTANDAO WAKE NCHI NZIMA


AIRTEL YAZIDI KUPANUA MTANDAO WAKE NCHI NZIMA

Yaelekeza nguvu vijijini
Leo kanda ya ziwa na nyanda za kusini wanauhuru wa kuongea wakiwa na Airtel!
Dar es Salaam 08/09/2011, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa huduma bora za mawasiliano yasiyo na kukatika katika leo imeendelea kutimiza ahadi yake ya kufikisha mawasiliano vijijini

Airtel imethibitisha hayo kwa kufikisha huduma za mawasiliano vijijini.

Akiongea kuhusiana na hili mwenyekiti wa kijiji cha Ibililo bwana Jackson Ambilikile Kapoloso aliseme “tumefarijika kwa kufikishiwa huduma za mawasiliano hapa wilayani kwetu Rungwe wiki iliyopita. Airtel ni mtandao peekee unaopatikana maeneo haya, ni wazi na dhahiri mawasiliano haya yametufikia katika wakati muafaka sisi wakazi wa Rungwe na vijiji vinavyotuzunguka, hii itatusaidia kuongeza tija katika shughuli zetu za kijamii na uchumi kwa urahisi.
Hivyo basi tuko tayari kuamia Airtel! Aliongeza Ambilikile.

Akiongea na waandishi wa habari Meneja uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema “ Katika muendelezo wa mikakati ya kupanua na kuboresha mawasiliano nchini hivi karibuni tumefikisha mawasiliano katika vijiji mbalimbali kwa kuzindua minara ya mwasiliano saba mkaoni mbeya. Maeneo tuliyoyafikishia huduma wiki iliyopita yatawafaidisha pia wakazi wa vijiji vya jirani.

Tunajisikia fahari kuwaunganisha watanzania kwani tunaona ni jinsi gani mawasiliano yanavyoweza kuleta mabadiliko katika maendeleo ya wananchi na nchi kwa ujumla, tunatambua Mawasiliano ni muhimu na si vinginevyo.
Alingeza Mmbando

Leo Airtel inazindua mawasiliano kanda ya ziwa kijiji cha Utegi , huduma hizi hapa Utegizitawafikia pia wakazi wa vijiji vya Koaki, Ingili, Bukwe, Nyanduga,Otuna, Buturi, Yagoro, Kanguge, Mangra wilayani Rorya mkoani Mara.
Kadri tunavyopanua wigo wa mawasiliano ndivyo tunavyochangia katika kuongeza ubora wa maisha kwa jamii na kuchangia maendeleo ya nchi. Airtel tunataka mawasiliano yaweze kufika kwa urahisi nchini kote.
Sasa wakazi wa Utegi na vijjiji jirani watapata huduma na bidhaa zetu kama kupiga na kupokea simu, huduma ya internet, na promosheni mbalimbali. Huu ni wakati muafaka kwa wakazi wa Ileje, Chunya, Tukuyu, Mwakareli, Rungwe, Mwanjelwa, Mbozi, Tunduma, Songwe, Uyole na Mbalizi, Ku HAMIA Airtel sasa” Alisisitiza Mmbando

Airtel inaendelea na Jitihada za kutanua mtandao wake ikiwa ni kampuni yenye mtandao bora na sasa inawateja zaidi ya million sita na laki tano nchi nzima.
Dhamira yetu Artel katika kupanua mtandao zaidi ni kuhakikisha tunafikia lengo la kutoa uhuru wa kuongea nchi nzima alimaliza kwa kusema Mmbando!


0 comments: