Social Icons

Sunday, August 7, 2011

ZIARA YA MKE WA RAIS WA BURUNDI YAZIDI KUSHAMILI BONGO

Mke wa Rais wa serikali ya mapinduzi Zanzaibar Mama Mwanamwema Shein (kulia) akimpatia zawadi mbalimbali Mke wa Rais wa Burundi Dkt, Denise Nkurunziza baada ya hafla ya futari katika Ikulu ya Zanzibar jana. Denise yupo katika ziara ya siku sita nchini .
Picha ya pamoja ya wake wa Marais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Dkt, Denise Nkurunziza wa Burundi pamoja na baadhi ya viongozi wa taasisi mbalimbali za wanawake Zanzibar.
Mwanafunzi Zainab Musa wa shule ya sekondari maalumu ya watoto yatima WAMA-NAKAYAMA inayoendeshwa na Taasisi ya WAMA iliopo Wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani akimuonyesha mazoezi ya vitendo katika maabara jinsi ya tofauti matumizi ya moto. Mke wa Rais wa Burundi Dkt. Denise Mucumi Nkurunziza (kushoto aliyevaa nguo ya brown) akiwa na Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA ,Mama Salma Kiwete.

PICHA NA MWANKOMBO/HABARI MAELEZO

0 comments: