Social Icons

Thursday, August 4, 2011

WANNE STAR ADAI KUTAPELIWA NA MUANDAAJI WA VODACOM MISS ARUSHA CITY CENTER

MSANII mahiri wa ngoma za asili Tanzania, Salum Wanne ‘Wanne Star’, anadai kutapeliwa na Bi. Sophia Urio ambaye muandaaji wa mashindano ya Miss Arusha City Center 2011 yaliyofanyika Mei 13, 2011 katika ukumbi wa Triple A, Arusha.

Akizungumza na MATEJA20 hii, Wanne Star alisema kuwa anasikitika sana kutapeliwa na muandaaji wa shindano hilo kwa kitendo cha kumukimbia mjini Arusha pindi alipoenda kufanya onyesho mashindano hayo.

Akisimulia mkasa huyo msanii huyo alisema haya, "Kikweli sikutarajia kama mwanana dada huyu angeweza kunitapeli, nilifika mjini Arusha na akatupokea vizuri na kutupeleka hotelini tukalala na siku yake ya pili tukaenda kufanya kazi, kuhusu malipo alisema atatupa wakati wa show itakapoisha ila baada ya show kuisha hakuonekana jambo ambalo lilitufanya tukawa na wasi wasi na kukampigia simu hakupokea na baadae akazima kesho yake simu yake haikupatikana kabisa hali ambayo ilitufanya tukaanza kuhangaika huku na kule,"

Aliongeza kuwa iliwabidi wamfuate Dj Charles Muhamiji na kuwapatia nauli na kufanikiwa kurudi jijini Dar es Salaam.

Nilipomuuliza ni njia gani ambazo amezifanya ili kuweza kupata hela zake, msanii huyo alianza kusononeka kwa kuonyesha sura ya huzuni na kusema kuwa yote anamwachia Mungu kwa vile jasho la mtu huwa halimwagiki bure.

"Nilichojaribu kufanya mawasiliano nae nampigia simu japo mpaka hivi sasa nikimpigia hapatikani na nimesononeka sana kwa kitendo ambacho amenifanyia.

Katika mahojiano yaliyofanywa na MATEJA20 hii na washiriki walioshiriki mashindano hayo wamelalamika kutolipwa pesa zao jambo ambalo halikuonyesha utu.

Mmoja ya washiriki wa mashindano hayo ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema kuwa mpaka sasa hawajalipwa kitu na hawajui mustakabali wa malipo yao.

"Tumechoka mpaka sasa hatujalipwa na hatujui itakuwaje kuhusu malipo yetu ndiyo maana tumeleta kilio chetu kwenye vyombo vya habari ili viweze kutusaidia," alisema mshiriki huyo.

Nae kijana mmoja ambaye hakupenda jina lake litajwe alisema kuwa yeye amefuatilia malipo yake kila akipiga simu majibu yake huwa nitakulipa nitakulipa mara aambiwe hela yote amelipa deni Naura Springs hoteli jambo ambalo limekuwa likimkera mara kwa mara.

"Nimejaribu kumpigia mara kwa mara na kumuuliza kuhusu deni langu yeye husema oh! Vodacom walitoa tu, Milioni 2 na hela yote nililipa deni hoteli ya Naura Springs, Arusha,"

Mpaka sasa ni miezi miezi miwili tokea mashindano hayo yamefanyika na baadhi ya watu wamekuwa wakilalamikia kutolipwa hali ambayo inaonyesha dhahili ni kutapeliwa.

MATEJA20 hii imesikitishwa na malalamiko ya washiriki wa mashindano mbali mbali kwa watu ambao wamekuwa wakiandaa mashindano mbali mbali kuwa baada ya kumaliza mashindano yao huwa wanawakimbia bila kuwalipa.washikiriki kwa kutowalipa chochote.

0 comments: