

t












TATIZO la Ukosefu wa Nishati ya Mafuta wazidi kuitesa nchi kutokana na kuwa adimu, ambapo baadhi ya wamiliki wa vituo vya mafuta wanadaiwa kuitisha mgomo baridi, kwa kisingizio ya nishati hiyo kutopatika kwenye visima vya mafuta wanakochukulia.
Mateja20, jioni hii ilipita mitaa ya Sinza Mori katika kituo cha Big Born na kukuta kasheshe la aina yake ambapo Askari polisi wakiwa wamemkwida muungwana mmoja baada ya kuvuka foleni na kusonga kwa mbele zaidi akitaka kumiminiwa mafuta kwenye releni yake ili awahi usafiri wake uliyokuwa umemzimikia, barabarani na juhudi zake hizo kuishia mikononi mwa maafande waliyokuwa wametanda kwenye kituo hicho kwaajili ya usalama, na kuelekeza foleni ya magari yaliyokuwa yakielekea kituoni hapo tayari kwa kupata mafuta ambayo pia yalikuwa yakitolewa kwa sharti la kutozidisha lita 20.
Pamoja na hilo katika kituo hicho kulikuwa na mafuta aina ya Petrol tu huku Diesel ikiendelea kuwa tatizo kubwa pande hizo ambapo magari yaliyohitaji huduma hiyo yaliishia kupanga foleni.
0 comments:
Post a Comment