Social Icons

Thursday, August 4, 2011

MKE WA RAIS WA BURUNDI AITEMBELEA WAMA

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete (kulia) akimkabidhi vipeperushi vya Taasisi yake Mke wa Rais wa Burundi, Mama Denise Bucumi, alipotembelea katika Ofisi za Taasisi hiyo jana, jijini Dar es Salaam, ambapo alifanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ya wanawake na watoto pamoja na masuala mengine ya kijamii, Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.
Mke wa Rais wa Burundi, Mama Denise Bucumi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Taasisi ya WAMA jijini Dar es Salaam jana baada ya kufanya mazugumzo na Mwenyeji wake mke wa Rais Mama Salma Kikwete.

0 comments: