Social Icons

Wednesday, August 3, 2011

FUTARI YAFANA KWA PAPA YUSUPHED M/NYAMALA

Zung Fedha (kushoto), na Kigogo Paul (kulia) wakitupia kitu cha futari pale kati na wageni waalikwa.
Da' Samirah akiandaa mahanjumati muda mfupi kabla ya watu kukandamiza futari hiyo.
Mama Yusuphed na mwanaye Rahma wakifuturu


Wageni waalikwa wakitupia vyuku pale katiRahma Yusuphed akikaribisha wageni kwa ukarimu nyumbani hapo
Wadau wakiwa tayari kwenye kitu cha mkeka wakisubiri adhana tayari kwa kufuturu

JIONI ya leo Mateja20 nilikaribishwa pande za Mwananyamala Kisiwani kwenye bonge la futari katika familia ya Papaa Yusuphed. Mpango mzima ulihudhuriwa na watu kibao ikiwa ni spesho kwa ajili dua ya marehemu wote wa familia hiyo ambapo zoezi hilo litaendelea hadi mfungo utakapomalizika. Mwaliko huo ulikuja kutoka kwa Mamaa Yusuphed ambaye ni dada wa Shakoor Jongo 'Zung Fedha'. Watu wote mnakaribishwa katika familia hiyo kila siku muda wa kuturu.

0 comments: