skip to main |
skip to sidebar
BSS YAZIDI KUNOGA, WAWILI WAINGIA DANGER ZONE, MWAPWANI ACHAPA RAPA!
Mwapwani Yahya, akiimba kwenye kinyang'anyiro hicho muda mfupi baada ya kusomewa matokeao, ambapo aliaga mashindano hayo.
Mshiriki kutoka pande za Mwanza, Beatrice William, akimkumbatia kwa hudhuni Mwapwani Yahya, mara baada ya kutolewa kwenye shindano hilo.
Waziri Salum, naye hakuwa nyuma kumuaga Mwapwani baada ya kuchapishwa rapa.
Mtangazaji wa shindano hilo, Godwin Gondwe akitaja washiliki waliyoingia kwenye danger zone.
Mwapwani Yahya (kulia), akionyesha huzuni na washiriki wenzake waliyoingia kwenye danger zone ya shindano hilo.
Bella Kombo (kushoto), akiwa kwenye pozi na Beatrice William (kulia), na mshiriki mwenzao aliyeingia kwenye danger zone Imani Lisu aliyekaa kushoto na Mwapwani Yahya.
Sarafina Mshindo, akitetea nafasi yake kwenye kinyang'anyiro hicho.
Mary Banyuka, akiwajibika jukwaani.
Mary Lukosi akiwa shughulini.
Chiby Dayo (kulia), akibadilishana mawazo na Rogers (katikati), na Waziri Salum kushoto, muda mfupi baada ya mpambano huo kuanza.
Watangazaji wa shindano hilo, Bob Junior (kushoto), na Godwin Gondwe wakiwa kwenye pozi mara baada ya kuhitimisha ishu hiyo.
Bella Kombo naye akitetea nafasi yake jukwaani hapo.
Beatrice William, akionyesha makeke yake jukwaani hapo.
Chiby Dayo akionyesha swagger za kihindi jukwaani hapo.
Imani Lisu akipagawisha jukwaani hapo.
Mwanamuziki wa bendi ya African Stars International 'Twanga Pepeta', Haji Ramadhani, akitetea jina la bendi yake kwenye mashindano hayo.
Bella Kombo katika pozi.
Godwin Gondwe, akiendelea na ratiba zake jukwaani hapo.
Waamuzi wa shindano hilo, Banana Zorro (katikati), akifuatilia mchakato huo na Salama Jabir (kushoto), na Master Jay.
Mshiriki wa shindano hilo anayetumia gitaa, Rogers, akipagawisha jukwaani hapo.
Mshiriki wa shindano hilo Waziri Salim akiwajibika kutetea nafasi yake.
MPAMBANO wa kumsaka mshindi wa shindano la Bongo Star Search Second Chance 2011, unazidi kupamba moto kwa washiriki wake kuendelea kupigana vikumbo kila kukicha,
Katika shindano hilo, washiriki wawili waliingia kwenye Danger zone, ambaye ni Mary Banyuka na Imani Lisu,huku Mwapwani Yahya akiyaaga mashindano hayo.
Hadi sasa wamesalia washiliki 10, wanaowania nafasi hiyo, na hakuna mwenye sifa za kumshinda mwenzake hadi sasa, hivyo suala hilo linawapa wakati mgumu majaji wa kinyang'anyiro hicho.
0 comments:
Post a Comment