Vimwana hao wakiwa jukwaani tayari kwa kuonyesha umahairi wao.
Mmoja wa washiriki wa shindano hilo, Mary Hamis, akionesha manjonjo yake stejini.
VIMWANA Manywele Twanga Pepeta, usiku wa Jumapili walifanya makubwa ndani ya ukumbi wa Klabu ya TCC Chang’ombe, Temeke, jijini Dar es Salaam, kwenye shoo ya utambulisho kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Utambulisho huo ulisindikizwa na Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta Sugu Kisima cha Burudani’ ambapo walikonga vilivyo nyoyo za mashabiki waliokuwa wamefurika ukumbini hapo kushuhudia shoo hiyo.
Akizungumza na paparazi wa mtandao huu, Mratibu wa shindano hilo Maimartha Jesse, alisema shoo hiyo ilikuwa mahsusi kwa wakazi wa pande hizo, ikiwa ni utangulizi kabla ya kuifikia siku ya fainali ya shindano hilo itakayofanyika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza, Julai 8 mwaka huu.
Amina naye hakuwa nyuma kuonyesha ‘swaga’ zake.
Maimartha Jesse akiongea jambo kwenye utambulisho huo.
Wanenguaji wa kike wa ‘Twanga Pepeta’ wakifurahia shughuli hiyo.
0 comments:
Post a Comment