Na Mwandishi Wetu
Mwanadada aliyewahi kuwa Mtangazaji wa Televisheni ya Channel 5 kisha akapata zali la kuolewa na Mzungu nchini Marekani, Teddy Kalonga ‘TK’ (pichani) amewashangaza mashabiki wake kufuatia kuanika picha yake ikionesha kuwa ni mjamzito.
Picha hiyo ambayo pia inapatikana kwenye blog yake inamuonesha TK ambaye pia anajishughulisha na ‘umodo’ akiwa na ‘kitumbo’ ambacho kwa haraka kinaonekana kuwa na zaidi ya miezi minne.
Wakiuzungumzia ujauzito huo, mashabiki mbalimbali wa mwanadada huyo walimpongeza kwa hatua hiyo lakini wakamlaumu kwa kuwaficha hadi mimba yake kuwa kubwa.
“Mimba imempendeza sana lakini mbona katuficha sisi wadau wake? Mungu amjalie ajifungue salama na ikiwezekana apate mapacha,” alisema Karen wa Moshi.
Naye Miriam Simbeyu wa Kinondoni jijini Dar alisema: “Nami sijui nitakuwa lini kama alivyo TK, mimba ni kitu kizuri sana hasa kwa walio katika ndoa…furaha ilioje kwake.”

0 comments:
Post a Comment