Social Icons

Sunday, June 19, 2011

Global Publishers SEMINA YA CHANGAMOTO NA NAFASI KATIKA BIASHARA YA MAFUTA YA MAWESE DUNIANI…!!!


Mwakilishi wa Ubalozi wa Malaysia nchini Tanzania Bw. Kathiravan Subramaniam akifungua semina ya Masoko ya Mafuta ya Mawese iliyofanyika kwenye Hotel ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam.


-Afisa Mkuu Mtendaji Msaidizi wa Kampuni ya MPOC Dkt. Kalyana Sundram akiwasilisha mada ya kwanza juu ya kuimarisha bidhaa za vyakula kwa bara la Afrika katika semina iliyofanyika kwenye Hotel ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar.


Mkuu wa Idara ya Utafiti na Maendeleo aishie nchini Afrika Kusini Dkt. Aubrey Parsons ambaye aliwasilisha mada ya pili juu ya nafasi mbali mbali za mazao ya Mawese kwa bara la Afrika.


Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa MPOC Bw. Faudzy Asrafudeen, Afisa Mkuu Mtendaji Msaidizi wa MPOC Dkt. Kalyana Sundram sambamba na Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL Bw. Vijay Raghavan kwa pamoja wakifuatilia semina hiyo.


Mkurugenzi wa Masoko wa MPOC Bw. Faudzy Asrafudeen akiwa anatoa mada ya tatu juu ya Maendeleo ya Kiwanda cha Mafuta ya Mawese pamoja na Masoko kwa Dunia.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mjini Mh.Mohammed Dewji (kushoto) sambamba na Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL Bw. Vijay Raghavan (katikati) wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Viongozi wa MPOC kutoka Malaysia kwenye Hotel ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam.

0 comments: