Social Icons

Saturday, June 18, 2011

BONGO MOVIES WAVAMIA DOM

Vincent Kigosi ‘Ray’ (katikati), Rado (kushoto) na Single Mtambalike ‘Richie’ kwenye kambi hiyo, African Dream Hotel, Area E, Dodoma. PICHANI JUU: Kuanzia kulia ni Cloud, Wema, Viva, Jacq Pentzel, Suleiman Barafu na Aunt Ezekiel.

Wema na Jack


Na Luqman Maloto, Dodoma
Klabu ya michezo ya wasanii wa filamu Tanzania, (Bongo Movie Club) ipo tayari kuwakabili Timu ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Bunge Sport Club) leo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa.
Mechi ya kirafiki, ina lengo la kukuza ushirikiano, umoja na upendo kati ya wabunge na wasanii wa filamu Tanzania.


Global Publishers ipo mjini Dodoma na jana jioni, ilitembelea kambi ya Bongo Movie ambayo ipo kwenye Hoteli ya African Dream, Area E.


Kwa jumla, wasanii wamejigamba kuitoa nishai Bunge Sport Club.
Leo, kutakuwa na mechi mbili, mpira wa miguu na netiboli ambazo zitachezwa muda mmoja.
Msemaji wa Bongo Movie FC, Steve Kanumba alisema kuwa wachezaji kwenye ari ya kutosha na hakuna majeruhi.


Aliwataja wachezaji wa soka kuwa ni Vincent Kigosi ‘Ray’, Musa Issa ‘Cloud’, Deogratius Shija, Steve Nyerere, Kanumba na wengineo.


Netiboli, wachezaji ni Aunt Ezekiel, Wema Sepetu, Jacqueline Pentzel, Zuwena Yusuf ‘Shilole’ na wengineo.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Sport Club, Amos Makalla ‘Fabregas’ alisema kuwa lazima watawafunga Bongo Movie kwa sababu wao hawatacheza mpira wa kibishoo.

Aliwataja wachezaji wa soka kuwa ni Peter, Chris na Kadebe ambao ni wafanyakazi wa bunge pamoja na waheshimiwa Godfrey Zambi, Yusuf Masauni, William Ngeleja, Makalla ‘Fabregas’, Lameck Mwigulu, Abdallah Haji na wengineo.

Netiboli, ni waheshimiwa Mwanahamisi Kombo, Grace Kihwelu, Jenista Mhagama, Kidawa Hamis, Ester Matiku na wengineo.

0 comments: