Waandaji wa tamasha hilo wakiwa tayari kuongea na mwaandishi wa habari.
Mmoja wa waanzilishi wa Ziff, Bi. Fatuma Aloo, akiongea jambo na waandishi.
TAMASHA la Filamu la Kimataifa la Zanzibar (Ziff) linalofanyika kila mwaka visiwani humo linatarajiwa kufanyika Juni 18 hadi 26. Waandaji wa tamasha hilo waliyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari leo katika Hoteli ya Movenpick ya jijini Dar es Salaam, ambapo walielezea mchakato mzima wa tamasha hilo linalowajumuisha wacheza filamu mbalimbali wa ndani na nje ya nchi. Katika tamasha hilo pia atakuja mwanamuziki mkali wa Reggae kutoka Jamaica, Orville Richard Burrell ‘Shaggy’ na mwanamuziki kutoka Zimbabwe, Oliva Mtukudzi.
Mkurugenzi wa sasa wa Ziff, Ikaweba Bunting, akizungumza jambo.
Mkurugenzi wa zamani wa ZIFF, Martin Mhando, ambaye kwa hivi sasa ni mmoja wa wanakamati ya Ziff nae akitoa machache.
Meneja wa Kampuni ya Bia ya Tusker ambao ni mmoja wa wadhamini, Bi Ritha Mchaki, akielezea jinsi watakavyoendesha promosheni yao visiwani humo.
0 comments:
Post a Comment