Bw Sixtus Mapunda
Kuna taarifa za ndani kabisa kutoka ndani ya chama cha Mapinduzi CCM kuwa, Bw Sixtus Mapunda ameteuliwa kuwa msaidizi wa Nape Nnauye yaani katibu msaidizi mkuu idara ya itikadi na uenezi blog yako hii namba moja ya kisiasa ina habari kamili.
Akiongea na blog hii, Bw Sixtus Mapunda ambaye kabla ya uteuzi huu alikuwa mmoja wa viongozi wa CCM wilaya ya Kinondoni amekiri kuwa ni kweli amepata barua ya kuteuliwa kushika wadhifa huo ambao kwa maneno yake anasema...." nimepokea kwa furaha uteuzi huu na naahidi kushirikiana na Wanaccm wenzangu ili kuijenga CCM na taifa letu..." pia Bw Mapunda hakusita kuweka wazi msimamo wake kwa kile kilichotokea Dodoma huku akipongeza uamuzi wa CCM kujitathimini na kuanza kuchukua hatua stahiki.
Uteuzi huu unatafsiriwa na wengi ni kama hatua ya CCM kuamua kuwaongezea nguvu vijana hasa Nape, January na wengine ili kukijenga upya chama hasa kwa kupambana na kile kinachoitwa ufisadi ndani ya chama hicho.
KWA HABARI ZAIDI TEMBELEA www.novatzdream.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment